Thursday, March 1, 2012

SENEGAL ; MACKY SALL, asema yuko tayari kumvaa Mkongwe, WADE ,kwenye duru ya pili

Kushoto,, Macky Sall....kulia ni Rais Wade

Wakati wadadisi wa mambo ya siasa za Senegal wakisema rais Wade atakuwa na kibarua kigumu katika duru ya pili ikiwa upinzani utaungana dhidi yake.

Mpinzani wa Rais wa pili kwa ukubwa wa umri barani Afrika, ukimwacha Rais Mugabe, Bw,Macky Sall amesema yuko tayari kukabiliana na rais Wade na kuongeza kuwa upinzani umeshinda viti vingi zaidi vya ubunge.

Katika awamu ya kwanza ya Uchaguzi, Bwana Wade alipata asilimia 35 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumapili. Rais huyo sasa atachuana na aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo wakati wa utawala wake Macky Sall ambaye alipata asilimia 26 ya kura zote zilizopigwa.

Tayari tume ya uchaguzi nchini Senegal imesema kuwa kutakuwepo na duru ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, kushindwa kuzoa kura za kutosha kutangazwa mshindi wa moja kwa moja katika duru ya kwanza.

Hata hivyo Bw, Wade, ameelezea matumaini ya kunyakua tena uongozi wa nchi hiyo.


No comments: