Friday, February 24, 2012

HUKUMU YA SAMAKI WA MAGUFULI: WAWILI JELA MIAKA 20


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh Bilioni 21 kwa washitakiwa wawili Raia wa China waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haram katika Bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania.
Kesi hiyo iliyokuwa maarufu kama kesi ya samaki wa magufuli leo imefikia tamati baada ya hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Agustino Mwalija ambaye pia aliwaachia huru washitakiwa wengine watatu.
Waliopewa adhabu hiyo ni Nahodha wa meli hiyo ya Tawaliq 1, Hsu Chin Tai kwa mashitaka yote mawili ambayo ilikuwa ni uvuvi haramu wa samaki katika Bahari Kuu ya Tanzania bila kuwa na kibali. Na shitaka la pili akiwa pamoja na wakala, Zhao Hanquing.
Shitaka la pili ni la kuchafua mazingira ya bahari kwa uchafu wa samaki na mafuta ya meli.

Jaji Mwalija ametamka kuwa meli iliyotumika kwa uvuvi huo ambayo inadaiwa kuanza kutitia, serikali iitaifishe.
Mahakama hiyo pia imesema samaki kwasababu serikali iliwagawa bure mahakama hiyo imeridhia.Mahakama hiyo imesema kuwa nahodha anahusika zaidi kwa mashitaka yote kwasababu anatakiwa kabla ya kuanza uvuvi ajue vibali vyote vimekamilika.
Hata hivyo walipokamatwa walitoa vibali ambavyo vinaonyesha jina tofauti na lililoandikwa kwenye meli na vilikuwa vimeisha muda wake.
Washtakiwa hao wakiwa na wenzao walikamatwa na timu ya doria ya nchi tatu ambazo ni pamoja na Tanzania, Kenya Msumbiji na Afrika Kusini, Machi 8 mwaka 2009 wakiwa na tani zaidi ya 196 za samaki wa aina mbalimbali.

No comments: