Monday, August 22, 2011

MTWARA

IMANI POTOFU ZA PUNGUZA WANAOENDA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI

Imeelezwa kuwa kasi ya upimaji wa virusi vya ukimwi imepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha awali wakati ugonjwa huo unaanza kushika kasi ya maambukizi hapa nchi..
Hayo yamesemwa na muuguzi mkunga wa Taasisi ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi UMAT iliyoko mkoani Mtwara Bi, Anna Paulo alipokuwa akizungumza na Info radio ofisini kwake juu ya swala zima la kasi ya upimaji wa virusi vya ukimwi.
Muuguzi huyo amezitaji sababu za kupungua kwa kasi hiyo kuwa ni kutokana na wingi wa matabibu waliojitokeza wanaosadikiwa kutibu magonjwa sugu ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Amesema kuwa uwepo wa matabibu hao kumepelekea watu kuamini kuwa wanaweza kupona kwa kutumia dawa zao, na hivyo kupelekea watu wengi kuwafuata na kuacha kwenda kupima kabla ya kwenda kupima na kuthibitishwa kuugua ugonjwa huo.
Bi Anna amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kupima virusi vya ukimwi ilikujua afya zao na iwapo watagundulika kuwa na virusi vya ukimwi waweze kupatiwa dawa ambazo zitawawezesha kuishi kwa matumaini.

DODOMA

WANANCHI KUENDELEA KUPEWA ELIMU JUU YA UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA MAJI

Wizara ya maji katika mwaka wa fedha 2011/2012, imesema itatoa mafunzo ya usimamizi wa utekelezaji wa program za maji na usafi wa mazingira vijijini, kupiatia jumiya zitakazo sajiliwa zitakazowashirkisha wanaume na wanawake.
Hayo yamesemwa na waziri Stephene Wasira wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizra ya maji kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo Profesa Mark Mwandosya , kwa mwaka 2011/2012, bungeni mjini Dodoma hii leo.
Waziri wasira amesema wizara hiyo imeeandaa mpango wa kuelimisha jamii juu ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri huduma na mfumo wa maji, na pia kuelimisha juu ya mipango ya sekta ya maji kwa kipindi kijacho na kuainsha mafaniko na changamoto ambayo sekta hiyo imekabiliana nayo tangu mwaka 1961.
Katika michango yao wabunge wamesema kuwa matatizo ambayo yamekuwa yakiikabili nchi ni vyema yakapatiwa ufumbuzi wa haraka kwa kutekeleza miradi kadhaaa ya maji ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiorodheshwa na kutajwa na serikali kila mara bajeti zinapowasilishwa.
Wizara hiyo imeomba jumla ya sh. Billion 446, 94 million, 936 elfu kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo , ambapo kati ya fedha hizo,billion 17, million 455, 673 elfu kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati sh. billion 11, million 868, 805 elfu ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na billion 5, 587, 468 kwa ajili ya matumizi mengine.
Kwa mujibu wa waziri wasira Bajeti ya maendeleo inajumla y ash, billion 428, million 638, 963 elfu, ambapo kati ya fedha hizo shilling billioni 387 ni za nje

No comments: