Monday, August 22, 2011

DODOMA

MKE WA MBUNGE AFARIKI

Mbunge wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Baraza la Wawakilishi, Mussa Khamis Silima, amenusurika kufa kufuatia ajali mbaya ya gari akiwa na familia yake.
akitangaza taarifa hiyo mara baada ya dua kuliombea bunge na taifa , hii leo bungeni mjini Dodoma, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuwa, ajali hiyo ilitokea saa mbili kasorobo jana usiku, maeneo ya Nzuguni mkoani Dodoma.

Amesema kuwa katika ajali hiyo Mbunge huyo aliumia, kalazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma huku mke wake Mwanahweri Twalib akifariki dunia papo hapo,
Kwa mujibu wa Makinda, Mbunge na familia yake walikuwa wanarudi Dodoma wakitoka Zanzibar kumzika kaka wa mke wa Mbunge huyo. Makinda amewaeleza wabunge kuwa, mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kusafirishwa leo majira ya saa tano asubuhi kwa ndege kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya maziko ambayo yanefanyika alasiri ya leo. Mbunge huyo amelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uangalizi wa karibu wa kitaalamu.

No comments: