Monday, July 25, 2011

SIKU YA MASHUJAA YAADHIMISHWA LEO JULY 25 MKOANI MTWARA

Sehemu ya Makaburi 29 ya Mashujaa, huu ni upande wa waislamu


Sehemu ya Makaburi 72 ya Mashujaa, huu ni upande wa wakristo


MASHUJAA DAY

  • Rais Kikwete , awa mgeni rasmi
  • Leo jioni atawahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara, katika viwanja vya mashujaa

sherehe za maadhimisho ya siku za mashujaa zimefanyika leo mkoani Mtwara ambapo rais wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi, sherehe hizo zimekamilika hivi punde.

Katika hotuba yake futi mbele ya mamia ya wakazi wa mkoani Mtwara waliohudhuria maadhimisho hayo rais pamoja na mambo mengine ameelezea pia kusudi la siku ya mashujaa ambapo hapoa awali likuwa ikifanyika september mosi , amesema lengo ni kuiweka shughuli hiyo katioka sura ya kitaifa.

sherehe hizo zimefanyika mkoani mtwara kuwakumbuka mashujaa waliopigana katika vita vya kuikomboa Msumbiji kufuatia ukandamizwaji wa wakoloni wa kireno ambao waliwatesa sana wananchi.

Waziri wa mambo ya nje na ushikiano ushirikiano wa kimataifa Bw, Bernard Membe, amesema heshima nathamani ya damu za mashujaa zilizomwagika ni kubwa mno kuliko fedha zinazotumika kuandaa shughuli hiyo.

Mweneyekiti wa NCCR mageuzi Bw, James Mbatia kwa upande wake amesema hakuna haja ya kutumia gharama kubwa kuandaa shughuli hizi , na badala yake fedha hizo zingetumika kwa ajili ya kuhudumia na kushughulikia matatizo ya wananchi kama miundo mbinu ya maji, barabara, huduma za afya na kadahlika.

kuhusu shughuli hiyo kupewa umuhimu wa pekee na kuifanya kuwa siku ya mapumziko , waziri wa ulinzi Bw, Husein Mwinyi amesema ni wazo zuri ambalo serikali inaweza kulichukua na kulifanyia kazi, ingawa hapoa awali ilionekana ni vyema shughuli ama maadhimisho mengine yasiwe ya mapumziko ili kuona namna ya kuepuka athari za kiuchumi zinazoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Mbunge wa Mtwara Mjini Bw, Asnan Murji amesema kuwa ni vyema siku hii pia ikapewa umuhimu wa pekee, na hivyo ni vyema sasa taifa likaanza kufikria utaratibu mzuri wa kufanyika kwa sherehe hizi.

Jumla ya makaburi 101 ya mashujaa yapo mahali hapo , ingawa miili ya mashujaa 8 haikupatikana wakati makaburi hayo yalipohamishwa kutoka Msumbiji

No comments: