Saturday, July 23, 2011

DAR ES SALAAM NA MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu tarehe 25/07/2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa itaayofanyika kitaifa Naliendele, Mtwara.
Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Rais akiwa katika uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa Naliendele, atawaongoza viongozi wenzake kuweka silaha za asili katika mnara wa mashujaa.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Rais ataweka Mkuki na ngao, wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama ataweka sime na kufuatiwa na Kiongozi wa Mabalozi nchini ambae ataweka shada la maua, Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani ataweka upinde na mishale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion ataweka shoka.
Baada ya tukio hilo, kutakuwepo na sala kutoka kwa viongozi wa dini akiwemo Sheikh kwa niaba ya Waislam, Mchungaji kwa niaba ya C.C.T na Padre kwa niaba ya Roman Cathoric.
Aidha gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama litatoa heshima kwa Rais na kupiga wimbo wa Taifa kabla ya Rais Kikwete kutembelea makaburi na nyumba ya makumbusho ya Naliendele. Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

No comments: