Story ya Ahmad Nandonde, Musoma
Jumla ya wanafunzi 17,335 kati ya wanafunzi 45, 351
waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu mkoani mara wamefaulu mtihani wao wa
kujiunga na kidato cha kwanza huku wavulana wakiwa elfu 9,665 na wasichana elfu
7,670 sawa na asilimia 38.2.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo kaimu katibu tawala
mkoani mara bw. Buhacha kichinda amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana
ufaulu wa wanafunzi ulikuwa ni 26, 022 sawa na asilimia 56.8 baada ya serikali
kushusha alama za ufaulu na kuifikia 70 hadi 250 tofauti na mwaka huu ambao
umeanzia alama 100 hadi 250.
Aidha kaimu katibu tawala wa mkoa amesema katika kipindi cha
mwaka jana mkoa wa mara ulikuwa na asilimia 23.79 ya ufaulu tofauti na
mwaka huu ambapo mwanafunzi ameanzia alama 100 hadi 250 hali iliyopelekea
kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia 38.2.
Akizungumzia nafasi ya mkoa kitaifa bw. Kichinda amesema kwa
matokeo ya mwaka huu mkoa umeshuka toka nafasi ya 13 hadi ya 22 pamoja na
ufaulu kuongezeka.
Hata hivyo kichinda amesema serikali mkoani hapa inatarajia
kufanya kongamano kwa kubwa la elimu litakalowashirikisha wadau mbali mbali wa
Kwa lengo la kuinua hali ya ufaulu na kufikia kiwango cha awali ambapo mkoa wa
mara ulikuwa ukikamata nafasi za juu katika kiwango cha ufaulu nchini.
Kikao hicho cha kutangaza matokeo kilichowakutanisha wadau mbali
mbali wa mkoa, halimashauri za wilaya na manispaa kimefanyika jana (dec 28)
katika ukumbi wa mwekezaji uliopo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa mara.
No comments:
Post a Comment