Story yaAhmad Nandonde, MUSOMA
Idara Ya Uhamiaji Mkoani Mara Imefanikiwa Kuwakamata Wahamiaji Haramu Sita Raia Wa Ethiopia Kwa Kipindi Cha Kuanzia Nov Mosi Hadi Hivi Sasa.
Hayo Yamesemwa Leo Na Afisa Uhamiaji Mkoani Mara Bw. Ally Dadi Alipokuwa Akizungumza Na Mwandishi Wa Habari Hizi Ofisini Kwake.
Bw. Dadi Amesema Wahamiaji Hao Walikamatwa Wakiwa Kwenye Harakati Za Kuingia Nchini Kupitia Mpaka Wa Sirari Kuelekea Bunda Na Mwanza Kwa Kutumia Usafiri Wa Piki Piki.
Katika Tukio Hilo Amebainisha Kukamatwa Kwa Pikipiki Moja Iliyokuwa Na Namba Za Usajili T 861ckk Mali Ya Bw. Samwel Maduhu Mkazi Wa Bunda Mkoani Mara
Ametaja Baadhi Ya Majina Ya Wahamiaji Hao Kuwa Ni Tekla Eriwaro, Solomon Labso Abiwate Eldoro, Dopfe Huku Dereva Wa Pikipiki Hiyo Akikimbia Kusikojulikana.
Wahamiaji Hao Haramu Wameshitakiwa Katika Mahakama Ya Wilaya Ya Musoma Na Kesi Yao Imeahirishwa Na Raia Hao Kurejeshwa Rumande Baada Ya Kukosa Mkali Mani .
Pia Amebainisha Sababu Zinazowafanya Wahamiaji Haramu Kutumia Usafiri Wa Pikipiki Ni Kutokana Na Kuimarisha Ulinzi Katika Barabara Kuu Na Hata Katika Vizuizi. (MSIKILIZE BWANA DADI)
Hata Hivyo Amewataka Watenfaji Wa Kata, Vijiji, Wilaya Na Hata Kwa Wananchi Kuwa Na Uzalendo Kwa Kutoa Taarifa Katika Mamlaka Husika Pale Wanapowabaini Wahamiaji Haramu Au Wageni Ambao Wanawasiwasi Nao Katika Maeneo Wanayoishi.
No comments:
Post a Comment