Thursday, October 31, 2013
DAWA YA MBU KUPULIZWA MIAKA MITANO MFULULIZO MKOANI MARA
Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA.
SERIKALI MKOANI MARA KWA KUPITIA KITENGO CHA KUDHIBITI MALARIA NMCP CHINI YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI YA JAMII KWA KUPITIA MFUKO WA RAIS WA MAREKANI CHINI YA SHIRIKA LA MISAADA LA WATU WA MAREKANI USAID IMEAHIDI KUTEKELEZA MRADI WA KUPULIZIA DAWA MAJUMBANI KWA MIAKA MITANO MKOANI MARA.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MARA BW. JOHN TUPPA, MKUU WA WILAYA YA MUSOMA JACKSON MSOME AMESEMA MRADI HUO UNAOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA RESEARCH TRIANGLE INSTITUTE (RTI INTERNATIONAL) KWA KUSHIRIKIANA NA TIMU ZA USIMAMIZI UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA ZA MIKOA NA HALMASHAURI HIVI SASA UPO KATIKA AWAMU YA TATU HUKU WILAYA ZA BUTIAMA, BUNDA SERENGETI RORYA NA TARIME ZIKINUFAIKA NA MRADI HUO.
MRADI WA UPULIZIAJI DAWA YA UKOKO MAJUMBANI ULIOANZA 2010 MA KUATARAJIWA KUMALIZIKA 2015 UMELENGA KUPULIZIA KAYA 24,698 KATIKA WILAYA RORYA, SERENGETI NA TARIME KWA AWAMU HII HUKU WILAYA YA RORYA IKITEULIWA KWA MAJARIBIO YA UPULIZIAJI WA JAMII KWA KILOMETA ZISIZOPONGUA TANO ILI KUWAFIKIA WALENGWA NA KUPUNGUZA GHARAMA HUKU WAKITARAJIA MATOKEO MAZURI YATAKAYOSAIDIA KUENDELEZA ZOEZI HILO KATIKA WILAYA NYINGINE.
NAYE MRATIBU WA MALARIA NA MAGONJWA YA UWIANO MKOANI MARA MKOANI HAPA BI. TUKAE LISSO AMESEMA KUWA KUFUATIA KUANZA KWA MRADI WA UPULIZIAJI WA DAWA YA UKOKO HIVI SASA WAMEFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UGONJWA MALARIA KUTOKA ASILIMIA 30.4 MPAKA KUFIKIA 25.6 HUKU AKIAHIDI KUENDELEA KUPUNGUZA KASI HIYO YA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUO.
BI. LISSO AMEZITAJA BAADHI YA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO KATIKA UENDESHAJI WA MARADI HUO KUWA NI MAJI YANAYOTOKANA NA ZIWA VICTORIA IKIWA NI PAMOJA NA BAADHI YA WATU KUGOMEA ZOEZI HILO KUFANYIKA KATIKA MIJI YAO.
JUMLA YA WATOTO 946 WALIOCHINI YA MIAKA MITANO AMBAO SAWA NA ASILIMIA 25.0 WAMERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA KUTOKANA NA UGONJWA MALARIA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWEZI JANUARI MPAKA DEC MWAKA JANA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment