TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).
Serikali imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wa umma
itakayoanza kutumika mwezi huu, huku kima cha chini kikiongezwa kwa asilimia
41.18 kutoka Sh 170,000 hadi Sh240,000.
Waraka namba moja kwa watumishi wa umma uliotolewa na Katibu
Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi Julai 2 mwaka huu,
unaeleza kuwa marekebisho hayo ya mishahara yatahusu watumishi wa serikali kuu
na watumishi wa serikali za mitaa.
Wengine watakaonufaika na marekebisho hayo ni watumishi
walioshikizwa kwenye taasisi za umma na watumishi ambao watakuwa kwenye likizo
inayoambatana na kuacha kazi, kustaafu kazi au kumaliza mikataba baada ya Julai
mosi mwaka huu.
Waraka huo umeonyesha kuwa watumishi wa serikali ambao wanapata
mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya serikali hawatahusika
na marekebisho hayo.
Mei 29 mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, bungeni
mjini Dodoma, alisema Serikali imekamilisha majadiliano ya kuongeza kima cha
chini cha mshahara katika sekta 12 binafsi, kitakachoanza kutumika rasmi Julai
mosi.
Waziri Kabaka alitaja sekta hizo kuwa ni ya Ujenzi, Shule Binafsi,
Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma za Majumbani, Ulinzi Binafsi,
Madini, Afya, Uvuvi na Huduma za Majini, Usafirishaji, Mawasiliano na Kilimo.
Kwa mujibu wa Kabaka, mishahara imepanda kwa kiwango cha asilimia kati ya 21 na
65 huku Afya ikiongoza kwa kuongezwa ikifuatiwa na sekta ya hoteli na huduma za
nyumbani yenye asilimia 55.
Mei mosi mwaka huu akiwa mkoani Mbeya, Rais Jakaya Kikwete,
aliahidi unafuu wa maisha kwa wafanyakazi kwa kuangalia uwezekano pia wa
kupunguza kodi kwenye mishahara, Lipa Kadiri Unavyopata (PAYE).
Kuhusu kuongeza mishahara, Rais Kikwete aliahidi wafanyakazi
wote kwamba Serikali itaendelea kuiongeza kulingana na hali ya uchumi wa nchi.
Waraka huo unaonyesha kuwa mishahara mipya kwa watumishi wa serikali kada ya
masharti (operational service).
CHANZO : GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment