Nelson
Rolihlahla Mandela alizaliwa
18 July 1918. Mtu aliyejitwalia umaarufu mkubwa katika
harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi… lakini pia pamoja na kuipigania nchi
hiyo alikaa madarakani kwa muda mfupi zaidi 1994 to 1999. Mwafrika wa kwanza
kukaa ikulu ya Afrika kusini , akichaguliwa katika uchaguzi ulihusisha rangi
tofauti.
Serikali
yake ililenga kuondoa chembe chembe za ubaguzi wa rangi , umasikini na kuleta
usawa. Kwenye chama chake cha siasa African National Congress (ANC)
Mandela alikuwa rais kuanzia 1991 to 1997. Katika rubaa za kimataifa Mandela
alikuwa katibu mkuu wa vuguvugu la nchi zisizofungamana na upande wowote 1998
to 1999.
Kutoka
katika kabila la waXhosa alizaliwa
aktika familia ya kichifu, Mandela alisoma katika chuo kikuu cha
Fort Hare na chuo cha Witwatersrand, ambako
alisoma sheria . Wakati akiishi Johannesburg, alijiunga na ANC na
kuwa mwanzilishi wa Umoja wa vijana wa chama hicho.. Mnanmo mwaka 1948 chama
chama chake kilianza kutekeleza sera ya kuwa kinyume na ubaguzi wa rangi
umaarufuwa shujaa huyu wa Afrika ulianza kuonekana 1952 alipochaguliwa kuwa rais
wa tawi la Transvaal.. akifanya kazi kama mwanasheria alishitakiwa kwa
uanaharakati na kwa makosa ya uhaini Treason Trial 1956
to 1961 lakini alipatikana kuwa hana hatia.
Gereza
lililopo visiwa vya Robben Island na baadae gereza la Pollsmoor na
kasha gereza la Victor Verster yanabaki
na historia ya kukaa na mtu ambaye kwa sasa ni maarufu zaidi duniani kwa muda
wa mika 27.
Akiwa
rais wa ANC , Mandela aliongoza makubaliano na rais F.W. de Klerk kusitisha ubaguzi wa rangi na
kuitisha uchaguzi wa watu wa rangi zote mwaka 1994,
ambao yeye Mandela kupitia ANC alishinda. Akiwa rais , aliweka katiba mpya na
akaanzisha tume ya maridhiano , iliyopewa jukumu la kuchunguza makosa ya kwenda
kinyume na haki za binadamu.
Pamoja
na juhudi kubwa katika maendeleo ya taifa lake… Nelson Mandela alikataa kuwania kiti chake kwa mara ya pili…
akamwachia nafasi hiyo aliyekuwa makamu wake Thabo Mbeki, Mandela alianza kujihusisha na shughuli mbali
mbali na akitambuliwa pia kama mzee wa taifa hilo, shughuli zake zililenga
zaidi matendo ya ukarimu, hasa katika juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa
ukimwi kupitia mfuko wake wa Nelson Mandela Foundation.
Zaidi
ya tuzo 250 pamoja na tuzo ya amani ya Nobel , alizowahi kupokea Mandela ,
zilizohusisha kutambuliwa kwa mchango wake katika kupambana na ubaguzi wa rangi
na ukoloni... Anaheshimika zaidi Nchini kwake.. ambako anajulikana kwa jina la
Kixhosa MADIBA au TATA … majina hayo
yakimaanisha BABA… alitajwa pia kama BABA WA TAIFA … wengine barani Afrika
wanatamani kumtaja kama BABA WA AFRIKA
Leo
kiongozi huyu anatimiza miaka 95 .. ingawa yuko hospitali ambako madaktari
wanasema hali yake inaendea vyema …ingawa bado yupo mahututi.. dunia nzima inasherehekea
siku yake huku ikimtakia afya njema Mzee Madiba…
Twaungana
na dunia nzima kusema UWE NA AFYA NJEMA MADIBA !!!
No comments:
Post a Comment