Baraza la madiwani wa halmashauri ya
manispaa ya mtwara mikindani hii leo limeazimia kutowatoza ushuru kwaajili ya kushangia shughuli za elimu wafanya
biashara wadogo ili kuwapa nafasi zaidi
ya kujiendeleza kiuchumi.
Hayo yamejitokeza katika kikao cha
baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa wakati
madiwani pamoja na mambo mengine walipoketi kupitisha sheria ndogo ndogo za
halmashauri…Diwani wa viti maalum, Bi Zuhura Mikidadi wakati akichangia |
Akitoa mchango wake diwani wa viti
maalum Bi Zuhura Mikidadi amesema haifai kuwatoza wafanyaibiashara wadogo , akitolea mfano wa wauza samaki za kwenye mabeseni ushuru ambao utawaumiza...
Diwani wa kata ya Vigaeni Ally White amesikitishwa na kutotekelezwa kwa
sheria ambazo kila mwaka zimekuwa zikitungwa na kuwa na usimamizi mbovu..
Diwani wa kata ya Vigaeni Ally White wakati akichangia. |
Katika hatua nyingine Baraza hilo
limetoa muda wa hadi siku ya ijumaa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya manisapaa
kuhakikisha mkandarasi wa masoko mawili ya magomeni awe amepatikana..
Wakati akifunga kikao hicho Mstahiki
Meya wa manispaa Selemani Mtalika , amemwagiza mkurugeni kuona namna yoyote ile
ya kurekebisha barabara ya India kotaz…
PICHA ZAIDI KUTOKA KIKAO HICHO
No comments:
Post a Comment