Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA.
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU MKOANI MARA IMEMFIKISHA KATIKA MAHAKAMA YA MKOA ALIYEKUWA KAIMU AFISA MIPANGO MIJI WA MANISPAA YA MUSOMA BW. ANOLD ZEPHANIA NYAMBINA KWA KOSA LA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA KINYUME NA KIFUNGU CHA 31 CHA SHERIA YA TAASISI HIYO NAMBA 11/2007.
AKISOMEWA MASHITAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA TAKUKURU BW. MWEMA MELLA MBELA YA HAKIMU WA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MKOA BI. JANETH MSAROCHA AMBAPO MSHITAKIWA AMEKANA MASHITAKLA HAYO NA HIVYO KUACHILIWA HURU KWA DHAMANA.
AKITHIBISHA HAYO NAIBU MKURUGENZI WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA MKOANI HAPA BI. YUSTINA CHAGAKA AMESEMA JAN. 06 MWAKA JANA MSHITAKIWA NYAMBINA ALISHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA ARDHI AKIWA MJUMBE WA KAMATI HIYO ILIYOKAA KWAAJILI YA UGAWAJI WA VIWANJA VILIVYOKO BWERI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA.
AIDHA BI. YUSTINA AMESEMA KATIKA HICHO MSHITAKIWA AKIWA KAMA KATIBU ALIANDAA ORODHA YA MAJINA YA WATU WALIOPENDEKEZWA KUPATIWA VIWANJA NA KUWEKA MAPENDEKEZO YANAYOONESHA SIFA ZA MTU ANAYESTAHILI KUPEWA KIWANJA, NAMBA HUKU AKIWEKA JINA LAKE PAMOJA NA MAJINA YA WATUMISHI WENZAKE WA MANISPAA YA MUSOMA ILI KUPATIWA VIWANJA KATIKA MAENEO HAYO.
PIA KATIKA UCHUNGUZI HUO ULIIOFANYWA NA TAKUKURU UMEONESHA KUWA MSHITAKIWA HUYO HAKUINGIZA MAJINA YA AWALI YA WAKAZI WA MAENEO HAYO WALIOKUWA WAKIYAMILIKI MAENEO HAYO.
KUPITIA KIKAO HICHO MTUHUMIWA HUYO ALIJPATIA KIWANJA CHENYE NMABA 1378 KATIKA MAENEO YA BWERI KINYUME NA KIFUNGU CHA 15 (1) (3) NA (6)(A) CHA SHERIA SURA YA 113 KAMA ILIVYOFANYIWA MAPITIO MWAKA 2002.
No comments:
Post a Comment