Gharama za huduma za maji safi katika jiji la Mwanza zimeongezeka kwa asilimia 10, kutoka na kile kilichoelezwa kuwa ni kuifanya huduma hiyo iwe endelevu kutokana na kupanda kwa gharama za umeme…
Hayo yameelezwa na menejea uhusiano wa mamlaka ya maji safi na majitaka mkoani Mwanza (MWAUWASA) Bw, Robert Masunya, katika mahojiano maalumu na mwakilishi wa kituo hiki…
Kwa mujibu wa Bw, Masunya , ingezeko hilo linaanza mwezi huu baada ya mamlaka ya udhibiti wa maji na nishati EWURA , kukubali ombi lao la kupandisha gharama za maji….
MWAUWASA , imekuwa ikilipa Ankara kubwa ya umeme wa mitambo ya kusukuma maji inayofikia shilingi billion 2.3 kwamwaka , ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na kipindi kilichopita.
No comments:
Post a Comment