Wednesday, January 22, 2014

JINAMIZI LA AJALI, WANAFUNZI WANNE WAFARIKI DUNIA MKOANI MTWARA ASUBUHI YA LEO, 51 MAJERUHI

Kumetokea ajali jirani  na eneo la shule ya sekondari Mustafa Sabodo, eneo la Msijute mkoani Mtwara. Wanafunzi wamegongwa na gari wakati wakikimbia mchakamchaka. Huu ni mwendelezo wa matukio ya vifo yanayosababishwa na ajali za barabarani wiki hii.
Wanafunzi hao 4 ni wa jinsia ya kike, wanafunzi wengine saba kati ya majeruhi halizao zinatajwa kuwa mbaya zaidi. Mashuhuda wanasema ajali hiyo ilitokea wakati gari lililokuwa likitoka mtwara lilipokuwa likitaka kupishana na gari lililokuwa likitokea Masasi wakati wanafunzi wakiwa katikati yao, wanafunzi hao walipatwa na mshituko uliowafanya watawanyike.
Wakazi wa Mtwara walipofika katika Hospitali ya mkoa Ligula

No comments: