Sunday, October 20, 2013

GLORIOUS WORSHIP TEAM, LEO TENA WAMEFANYA SHOW KALI KATIKA KUSIFU NA KUABUDU NDANI YA JB BELMONT JIJINI MWANZA

Zimekuwa ni siku mbili za kukumbukwa kwa wapenda Kusifu na Kuabudu jijini Mwanza. Siku ya kwanza waliimba katika Campus night ya TAFES - SAUT Mwanza, Leo ilikuwa na siku yao tena ndani ya jiji la Mwanza mara hii wakiambatana na mkurugenzi wa Global Publishers Bw Erick Shigongo, ambaye pamoja na mambo mengine alikuwa msemaji pekee katika tamasha hilo la kusifu na kuabudu.
Vikundi vilivyoshiriki ni  CVCI, na TAFES -SAUT Praise team, kisha jukwaa likatawaliwa na GWT .PICHA tatu za juu ni wapenzi wa muziki wa injili wakiwa tayari wamechukua nafasi zao wakisubiri kuanza shughuli moja tuuuuuu....KUSIFU NA KUABUDU.

 PICHA hizi mbili, ni vijana wa TAFES - SAUT Praise team, wakishusha uwepo wa Bwana.

BAADAE SHUGHULI IKAHAMIA KWA GWT, ....
 Paul, akiimba pamoja na wenzake (GWT)
 Kawaida ya muziki wa injili huwa sio kumtazama mwimbaji, wooooteee mnakuwa watazamaji na waimbaji pia, maana zinapokolea sifa ukumbi unakuwa wima kama hivi.


 Erick Shigongo (Mwenye suti) hapa nae akirudisha sifa heshima na utukufu.
 PICHA YA CHINI NA YA JUU , Mabinti wa GWT wakimsifu Mungu

 Ninachokumbuka ahapa  ulikuwa unaimbwa wimbo wa UNAWEZA ...bonge moja la wimbo....Tunafanya utaratibu tutakuwekea video sooonnn!!!!!!!
 Mercy wa GWT
 Wakaka wa GWT

 Danny Kibambe...akiimba, (Behind the scene yake sasaaaaa..... wakati anajitambulisha akasema anapiga Kinanda hujawahi ona)
Erick Shigongo akiteta jambo na kiongozi wa GWT Emmanuel Mabisa

 ERICK SHIGONGO.... Ujumbe wake hapa ukawa ...ili uweze kufanikiwa ni lazima uanze kufanya jambo...lakini pia ili uweze kufanikiwa anza kufikiri na aina ya watu pia wanaokuzunguka, tafuta wale wa aina ambayo wewe unataka kufanana nao
 Kushoto Emma Solo , kulia Emma Bass.... hawa vijana wanakuja vizuri sana kiukweli kwenye hili eno la upigaji vyombo vya muziki.
 Sebene la Yesu likanoga sasaaaaaa..... 
Drama boy wa GWT ... piga sana ngoma huyu jamaaa leo...
Picha zote na ELIA MIGONGO, (Mr End Productions) Angalizo ikiwa utaamua kutumia picha hizi kwenye mtandao mwingine ruksa...

No comments: