Wednesday, August 28, 2013

UTATA RASIMU YA RASIMU YA KATIBA MPYA, KAMA ITAPITA LOWASA, DR. SLAA HAWAWEZI KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA..PIA HAIKO WAZI MAWAZIRI WATAPATIKANAJE

IBARA YA KATIBA MPYA PENDEKEZWA .... suala la mawaziri wetu...

IBARA 94.-(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa mawaziri au naibu mawaziri katika serikali ya jamhuri ya muungano:
(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge la Tanzania Bara, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar au madiwani kutoka Washirika waMuungano;
(b) mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanzania Bara au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SIFA ZA MTU KUWA WAZIRI  NI ZIPI KWA MUJIBU WA IBARA HII....ni hizi
94.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria za nchi;na
(b) angalau ana shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu kinachotambulika kwa mujibu wa Sheria za nchi.
....>>>  SHIDA HAPA NI HAWA MAWAZIRI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WATAPATIKANAJE ?
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KUTOKA KWA MAONI YA DOTTO BULENDU... UCHAMBUZI WAKE UKO HIVI..
Ibara ya 75(e) ya rasimu inasema ili kugombea nafasi ya uraisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mgombea anatakiwa kuwa na sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
Kwa mujibu wa Ibara ya 117(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuchaguliwa kuwaMbunge-(a) ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatuvya miaka mitano!.......
KWA MUJIBU WA MAONI YA DOTTO,...kama Ibara hii itaanza kuhesabu kuanzia sasa,Dk Silaa,Lowasa,Sitta na Membe hawatakuwa na sifa za kugombea Uraisi........je hii Ibara tumeiona?wale mlioko kwenye mabaraza hebu waulizeni watu wa tume wanamaanisha nini?
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
IBARA YA 92
(3) Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais
kuhusu mambo yanayohusu utekelezaji wa madaraka na matumizi ya
mamlaka ya Rais.
(4) Bunge naMahakama hazitakuwa na uwezo wa kisheria
kuchunguza kama ushauri wowote au ushauri wa aina gani ulitolewa na Baraza la Mawaziri.

No comments: