Friday, August 30, 2013

KIAMA KWA WANAOFUJA FEDHA ZA UMMA MUSOMA KINAKUJA

Story ya Ahmad Nandonde
LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA LIMEAZIMIA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WALE WOTE WALIOBAINIKA KUHUJUMU FEDHA ZA WATUMISHI WA SERIKALI WALIOFARIKI NA WALIOSTAAFU.
HAYO YAMESEMWA NA WAJUMBE WALIOHUDHURIA KIKAO CHA KAWAIDA CHA MADIWANI CHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA KILICHOFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA.
WAJUMBE HAO WAMESEMA ILI KUHAKIKISHA FEDHA HIZO ZINAREJESHWA WATU HAO WANATAKIWA KUFUATILIWA NA KUTAKIWA KUZIREJESHA FEDHA HIZO AMBAZO ZIMEKUWA ZIKITUMIKA KINYUME NA UTARATIBU ULIOPANGWA.
KWA UPANDE WAKE AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA JEREMIA NAMBUO AMESEMA KUWA KUFUATIA HUJUMA HIZO HALMASHAURI HIYO KUPITIA KIKAO HICHO CHA BARAZA KIMEAZIMIA KUZIREJESHA FEDHA HIZO KWA KUWABANA WAHUSIKA AMBAO HATA HIVYO WAMEAHIDI KUZIRESHA.
NAMBUO AMESEMA ILI FEDHA HIZO ZIREJESHWE KWA WAKATI, KIKAO CHA MENEJIMENTI KITAKAA NA KUTOA MAALUMU WA KUZIREJESHA FEDHA HIZO.
UHUJUMU HUO UMEBAINIKA KUFUATIA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA MDHIBITI WA HESABU ZA SERIKALI ILIYOPITIWA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2008 -2009

No comments: