Thursday, July 18, 2013

POLISI MARA WAIKALIA SIMBA KOONI

Story ya  Ahmad Nandonde,MUSOMA
Wakiwa katika ziara yao ya kanda ya ziwa klabu ya soka ya simba leo imeshindwa kuendeleza wimbi lake la ushindi kufuatia sare ya bao moja kwa moja na timu ya polisi mkoani mara katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya karume mjini musoma.
katika mchezo huo simba iliyouanza mchezo huo kwa kasi huku wakilishambulia mara kwa mara lango la polisi walitangulia kuandika bao lao kunako dakika ya 20 kwa mpira wa adhabu ndogo aliyochongwa na zahoro pazi na kumshinda mlinda mlango wa wa polisi mara.
kufuatia goli hilo simba waliendelea kulisakama kama nyuki lango la timu ya polisi lakini jitihada zote zilishindwa kuzaa matunda kwani waliweza kudhibitiwa vilivyo katika sehemu ya kiungo mkabaji aliyewahi kuitumikia klabu ya yanga miaka ya nyuma pastor mumbala kwa kuonesha mchezo mzuri na ufundi kwa mkubwa wa kumiliki sehemu hiyo ya kiungo.
hadi kipindi cha kwanza kinamalizika simba walikuwa wakiongoza kwa bao moja kwa bila.
kipindi cha pili kilianza kila timu ikijitahidi kucheza mpira wa kasi huku wakishambuliana na kwa zamu ambapo maafande hao wa mkoani hapa ndio walioonesha kulishambulia zaidi lango la simba na kufanikiwa kuikamata vilivyo timu ya simba hususan eneo la katika kiasi na hivyo kumfanya kocha wa simba jamhuri kihwelo maarufu kama julio kuongeza nguvu kwa kuwaingiza nasoro cholo, mussa mude, jonas mkude ambapo mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.
polisi walifanya mabadiliko kwa kumtoa pastor mumbala na nafasi yake kuchukuliwa na bonifas medadi ambapo mabadiliko hayo yialiifanya timu ya polisi kuongeza mashambulizi kwa kuliandama lango la simba na kufanikiwa kuandika bao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tano mpira kumalizika bao lililowekwa kimiani na kinda aliyeingia kuchukua nafasi ya pastor mumbala kufuatia kombora kali akiwa umbali wa mita 30 lililompita mlinda mlango wa simba na hivyo kuwa bao moja kwa moja.
mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa timu yua simba jamhuri kihwelo alioneshwa kuhuzunishwa kwake huku akimtuhumu refa katika mchezo huo kwa kusema kuwa hakuchezesha mchezo wa haki.
"huyu refa hakututendea haki kabisa kwani ametunyima penalt mbili za wazi na wachezaji wa polisi walikuwa wanaotea mara kwa marapia alikuwa akilikua offside nyingi za polisi kitu ambacho si sahihi kwa kanuni za uchezeshaji"....alisema julio.
kwa upande wake kocha watimu ya polisi ya mkoani hapa ommar hamis alionesha kufurahishwa na matokeo hayo huku akisema kuwa yamewatia moyo kwani ndiyo kwanza timu yake ilikuwa na wiki moja tangu kuingia kambini na hivyo kuutaka uongozi wa soka mkoani hapa (fam) kuiandalia timu hiyo michezo mingine ya kujipima nguvu itakayowawezesha kufanya vyema katika ligi ya (fdl)inayotarajia kuanza hivi karibuni.

No comments: