Thursday, July 18, 2013

HII NDIYO STORY FUPI YA MZEE MADIBA

Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa 18 July 1918. Mtu aliyejitwalia umaarufu mkubwa katika harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi… lakini pia pamoja na kuipigania nchi hiyo alikaa madarakani kwa muda mfupi zaidi 1994 to 1999. Mwafrika wa kwanza kukaa ikulu ya Afrika kusini , akichaguliwa katika uchaguzi ulihusisha rangi tofauti.
Serikali yake ililenga kuondoa chembe chembe za ubaguzi wa rangi , umasikini na kuleta usawa. Kwenye chama chake cha siasa  African National Congress (ANC) Mandela alikuwa rais kuanzia 1991 to 1997. Katika rubaa za kimataifa Mandela alikuwa katibu mkuu wa vuguvugu la nchi zisizofungamana na upande wowote 1998 to 1999.
Kutoka katika kabila la waXhosa alizaliwa aktika familia ya kichifu, Mandela alisoma katika chuo kikuu cha Fort Hare  na chuo cha  Witwatersrand, ambako alisoma sheria . Wakati akiishi Johannesburg, alijiunga na ANC na kuwa mwanzilishi wa Umoja wa vijana wa chama hicho.. Mnanmo mwaka 1948 chama chama chake kilianza kutekeleza sera ya kuwa kinyume na ubaguzi wa rangi umaarufuwa shujaa huyu wa Afrika ulianza kuonekana 1952 alipochaguliwa kuwa rais wa tawi la Transvaal.. akifanya kazi kama mwanasheria alishitakiwa kwa uanaharakati na kwa makosa ya uhaini Treason Trial 1956 to 1961 lakini alipatikana kuwa hana hatia.
Gereza lililopo visiwa vya Robben Island na baadae gereza la Pollsmoor na kasha gereza la Victor Verster yanabaki na historia ya kukaa na mtu ambaye kwa sasa ni maarufu zaidi duniani kwa muda wa mika 27.
Akiwa rais wa ANC , Mandela aliongoza makubaliano na rais F.W. de Klerk kusitisha ubaguzi wa rangi na kuitisha uchaguzi wa watu wa rangi zote mwaka 1994, ambao yeye Mandela kupitia ANC alishinda. Akiwa rais , aliweka katiba mpya na akaanzisha tume ya maridhiano , iliyopewa jukumu la kuchunguza makosa ya kwenda kinyume na haki  za binadamu.
Pamoja na juhudi kubwa katika maendeleo ya taifa lake… Nelson Mandela alikataa  kuwania kiti chake kwa mara ya pili… akamwachia nafasi hiyo aliyekuwa makamu wake Thabo Mbeki,  Mandela alianza kujihusisha na shughuli mbali mbali na akitambuliwa pia kama mzee wa taifa hilo, shughuli zake zililenga zaidi matendo ya ukarimu, hasa katika juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa ukimwi kupitia mfuko wake wa Nelson Mandela Foundation.
Zaidi ya tuzo 250 pamoja na tuzo ya amani ya Nobel , alizowahi kupokea Mandela , zilizohusisha kutambuliwa kwa mchango wake katika kupambana na ubaguzi wa rangi na ukoloni... Anaheshimika zaidi Nchini kwake.. ambako anajulikana kwa jina la Kixhosa  MADIBA au TATA … majina hayo yakimaanisha BABA… alitajwa pia kama BABA WA TAIFA … wengine barani Afrika wanatamani kumtaja kama BABA WA AFRIKA
Leo kiongozi huyu anatimiza miaka 95 .. ingawa yuko hospitali ambako madaktari wanasema hali yake inaendea vyema …ingawa bado yupo mahututi.. dunia nzima inasherehekea siku yake huku ikimtakia afya njema Mzee Madiba…
Twaungana na dunia nzima kusema UWE NA AFYA NJEMA MADIBA !!!


No comments: