Wednesday, July 31, 2013

DIWANI ATAKA WANANCHI WASITOZWE KODI ZA KUWAONEA

Baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya mtwara mikindani hii leo limeazimia kutowatoza ushuru kwaajili ya kushangia shughuli za elimu wafanya biashara  wadogo ili kuwapa nafasi zaidi ya kujiendeleza kiuchumi.
Diwani wa viti maalum, Bi Zuhura Mikidadi wakati akichangia
 Hayo yamejitokeza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa wakati madiwani pamoja na mambo mengine walipoketi kupitisha sheria ndogo ndogo za halmashauri…

Akitoa mchango wake diwani wa viti maalum Bi Zuhura Mikidadi amesema haifai kuwatoza wafanyaibiashara wadogo , akitolea mfano wa wauza samaki za kwenye mabeseni ushuru ambao utawaumiza...
Diwani wa kata ya Vigaeni  Ally White amesikitishwa na kutotekelezwa kwa sheria ambazo kila mwaka zimekuwa zikitungwa na kuwa na usimamizi mbovu..
Diwani wa kata ya Vigaeni  Ally White wakati akichangia.
Katika hatua nyingine Baraza hilo limetoa muda wa hadi siku ya ijumaa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya manisapaa kuhakikisha mkandarasi wa masoko mawili ya magomeni awe amepatikana..
Wakati akifunga kikao hicho Mstahiki Meya wa manispaa Selemani Mtalika , amemwagiza mkurugeni kuona namna yoyote ile ya kurekebisha barabara ya India kotaz…
PICHA ZAIDI KUTOKA KIKAO HICHO




No comments: