Tuesday, April 9, 2013

KAMA WEWE NI MDAU WA MIHOGO STORY HII INAKUHUSU


Story ya Ahmad Nandonde
IMEELEZWA KUWA ZAO LA MUHOGO KATIKA HALMASHAURI YA MUSOMA VIJIJINI LIMEENDELEA KUUGUA SIKU HADI SIKU KITU KINACHOPELEKEA NJAA KUTOISHA MIONGONI MWA WANACHI WA WILAYA HIYO.

HAYO YAMEBAINISHWA NA NAIBU KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA VIJANA WA CHAMA CHA WANANCHI CUF TAIFA, BW. THOMASI MALIMA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA RADIO VICTORIA FM.

MALIMA AMESEMA KUWA ZAO LA MUHOGO NDILO ZAO MAMA KATIKA JAMII YA WATU WANAOISHI VIJIJINI KATIKA MKOA WA MARA, KWANI WANALITEGEMEA KAMA ZAO LA CHAKULA NA BIASHARA, LAKINI SERIKALI KUPITIA WIZARA YA KILIMO NA USHIRIKA IMESHINDWA KUTAFUTA UFUMBUZI WA KUDUMU KATIKA KUTATUA TATIZO LA UGONJWA MIHOGO.

AIDHA AMESEMA KUWA HIVI SASA IPO KWA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KATIKA KULITAFUTIA UFUMBUZI TATIZO LA UGONJWA MUHOGO KAMA ILIVYOFANYIKA KATIKA MIKOA MINGINE KWANI MKOA WA MARA PIA UNAWAKULIMA AMBAO WANAPENDA KUONA SERIKALI YAO IKIWAJALI KWANI KWAKUTO KUFANYA HIVYO, NIKAMA WAKULIMA WA MUHOGO MKOANI MARA WAMETENGWA.
KATIKA UTAFITI WA MAGONJWA MASUMBUFU KWA ZAO LA MUHOGO ULIOFANYIKA MWEZI MAY MNAMO MWAKA 2011 ULIANGAZIA MIKOA YA MORORGORO, PWANI, TANGA, NA MTWARA PEKEE, NA KWAMBA KWA MUJIBU WA UTAFITI HUO KWA KUSHIRIKIANA NA VITUO MBALIMBALI VYA UTAFITI HAPA NCHINI VILIBAINI KUWA UGONJWA WA BATOBATO NDIO UGONJWA AMBAO UMEKUWA UKISUMBUA ZAO LA MUHOGO KWA KIASI KIKUBWA.

AIDHA MALIMA AMESEMA KUWA UGONJWA HUO BATOBATO UNAUTOFAUTI MKUBWA NA UGONJWA UNAOSUMBUA ZAO HILO KWA MKOA MARA, KWANI UGONJWA HUO KWA MKOA WA HUU UNAKULA MIZIZI NA SIYO MAJANI KAMA ILIVYO KWA BATOBATO.
TARIME

MAMLAKA YA MJI MDOGO WA TARIME MKOANI MARA IMEWATAKA WAFANYABIASHARA WANAOENDESHA SHUGHULI ZAO MAENEO YASIYO RASMI KATIKA SOKO KUU NA KITUO KIKUU CHA MABASI CHA MJINI HUMO KUONDOA BIASHARA ZAO MARA MOJA NA KUHAMIA KATIKA SOKO LA REBU ILI KUEPUKANA NA MSONGAMANO WA MAGARI NA WATU KATIKA MAENEO HAYO.

MTENDAJI MKUU WA MAMLAKA HIYO, HASHIMU BARONGO, AMEBAINISHA HAYO JANA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABRI OFISINI KWAKE KUWA WAMEFIKIA HATUA HIYO BAADA YA WAFANYABIASHARA HAO WAPATAO 400 KUGOMEA AGIZO LA SERIKALI LA KUHAMIA SOKO JIPYA LA REBU KWA VISINGIZIO VISIVYO VYA MSINGI.

AMESEMA OPERESHENI YA NGUVU KWA KUTUMIA MGAMBO NA POLISI INATARAJIWA KUFANYIKA MUDA WOWOTE KWA WALE WALIOKAIDI KUHAMIA SOKO HILO.

BARONGO AMESEMA OPERESHENI HIYO ITAANZA MUDA WOWOTE KUTOKANA NA MUDA ULIOTOLEWA KUMALIZIKA JUZI NA MSAKO UTAENDELEA DHIDI YA WALE WACHUUZI WANAOKAIDI KUHAMISHIA BIASHARA ZAO REBU, KWANI MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA YAPO NA VIBANDA VIPO VYA KUTOSHA NA KUONGEZA KUWA MFANYABIASHARA ATAKAE GOMA ATAPELEKWA MAHAKAMANI KWANI NI MUDA MREFU TANGU WATANGAZIWE KUHAMA ENEO HILO.

No comments: