Thursday, March 28, 2013

WAFANYA BIASHARA MUSOMA: BIASHARA IMESHUKA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA

WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU LA MUSOMA MJINI MKOANI MARA WAMESEMA KUWA, BIASHARA KWA SASA IMEKUWA NGUMU TOFAUTI NA ILIVYOKUWA HAPO MWANZO, KUTOKANA NA BIDHAA KUTONUNULIWA KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA.
WAFANYABIASHARA HAO WAMEYASEMA HAYO HII LEO WALIPOKUWA WAKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KWAMBA BIASHARA KWA SASA IMESHUKA KWA KIWANGO KIKUBWA KITENDO KINACHOSABABISHA KUKOSA FAIDA.
AKIFAFANUA KUHUSIANA NA BIASHARA HIYO KATIKA SOKO HILO MMOJA WA WAFANYABIASHARA HAO ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA LA KHADIJA HAMIS AMESEMA KUWA KWA SASA BIDHAA KAMA VILE NDIZI,NYANYA NA VINGINEVYO VINAOZA KUTOKANA NA KUKOSA SOKO, KITENDO KINACHO SABABISHA HASARA KUBWA KWA WAFANYABIASHARA HAO.
HATA HIVYO, MWENYEKITI WA SOKO HILO MACHOMAWILI AMEMALIZA KWA KUSEMA KUWA SUALA LINALOSABABISHA BIASHARA KUWA NGUMU SOKONI HAPO NI KUTOKANA NA MFUNGO WA KWARESMA KWA WAKRISTU KWANI KABLA YA MFUNGO HUO BIASHARA ILIKUWA NZURI.

No comments: