Saturday, March 2, 2013

STORY KUTOKA MUSOMA NA TARIME HIZI HAPA

Story za Ahmad Nandonde
MKUTANO kati ya serikali ya kijiji cha Nyangoto wilayani Tarime na wajumbe wa wa kikosi kazi cha Serikali ambacho kimeundwa ili kutafuta njia ya kumaliza migogoro ya wananchi na uongozi wa mgodi wa North Mara umevinjika bila ya kufikia muafaka.
Kuvunjiaka kwa mkutano huo kumetokana na wajumbe wa Serikali ya kijiji hicho kutoa mashari kuwa mazungumzo hayo yanaweza kufanyika hadi pale uongozi wa mgodi huo utakapofuta kesi ambayo inadaiwa kufunguliwa mahakama kuu jijini Mwanza.
Wakichangia katika mkutano huo ambao umedhuriwa pia na viongozi wa tarafa ya Nchage na kata ya Matongo,wajumbe hao wa serikali ya kijiji,wamesema mgodi huo umewafungulia wananchi zaidi ya 70 kesi wakiwataka kuhama katika maeneo yao bila kuwalipa fidia inayotakiwa hivyo kuendelea na mkutano bila kesi hiyo kufutwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Kufuatia madai hao kikosi kazi hicho kupitia kwa mwenyekiti wake Bw Adam Yusufu,kimesitisha kuendelea na zoezi hilo na kukubali kukutana na uongozi wa mgodi huo ili kuona namna ya kuindoa kesi hiyo na hivyo kutoa nafasi ya mazungumzo katika kutatua matatizo ya pande hizo mbili na kuleta amani katika eneo hilo.

Kikosi kazi ambacho kinaundwa na wajumbe kutoka wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi na vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa mara na wilaya ya Tarime,kitafanya kazi kwa kukutana na uongozi wa halmashauri ya tarime,baraza la madiwani la halmashauri ya tarime,wananchi wa vijiji husika na kupitia nyaraka mbalimbali zilizohusika katika ulipaji wa fidia katika kutatua migogoro hiyo.

MUSOMA
JESHI la polisi mjini Musoma mkoani Mara linawashilikia watu sita kwa kukamatwa katika matukio mawili tofauti ya wizi wa Nyaya za shirika la simu nchini TTCL na Copper Wire pamoja na mafuta ya Transfoma katika eneo la Bweri mjini Musoma.
Kamanda wa polisi mkoani Mara,kamishna msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma,amesema tukio la kwanza linawahusu Aloyce Alexander ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco mjini humo,Augustino Antony na Tuzo Adamu ambao kwa pamoja wamekamatwa baada ya kufanya hujuma ya wizi wa copper wire na mafuta katika Transfoma hiyo eneo la Bweri.
Kamanda Mwakyoma,amesema baada ya kupekuzi kufanyika watuhumiwa hao wamekutwa na baadhi ya vifaa ambavyo vimeibwa katika transfoma hiyo na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
Katika tukio la pili kamanda Mwakyoma amewataja Zena Othman,Eliabu Kuboja na Rajab Musa kuwa wakiwa katika gari lenye namba za usajili T 674 AJG wamekutwa tumbaku betri za minara 19 ya kampuni ya simu nchini na copper wire za Tanesco zenye uzito wa kilo 200 zikiwa zimehifadhiwa ndani ya magunia pamoja na vyuma chakavu mbalimbali.
Ameongeza kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa wamekiri kufanya kujihusisha na hujuma hizo katika mashirika hayo ya umma na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao.

No comments: