Wednesday, February 20, 2013

DUUUUHHHHHH>>>>>ASILIMIA 20 WAVUVI WANA VVU


Na Ahmad Nandonde,MUSOMA.
KUFUATIA TAKWIMU YA UKIMWI ILIYOFANYIKA MWAKA JANA KATIKA MAENEO YA WATU WANAOJISHUGHULISHA NA SHUGHULI ZA UVUVI IMEGUNDULIKA KUWA KARIBU ASILIMIA 20 YA WATU WANAOISHI KATIKA MAENEO HAYO WAMEATHIRIKA NA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI HIV.
HAYO YAMESEMWA NA MRATIBU UKIMWI MKOANI HAPA BW. EDWIN MWELEKA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA VICTORIA FM OFISINI KWAKE.
BW.MWELEKA AMESEMA KWA MUJIBU WA TAKWIMU ILIYOFANYIKA KATIKA KISIWA CHA LUKUBA KWA KUANDALIWA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI NCHINI NA KUDHAMINIWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAKE VICTORIA BASIN COMMISION IMEGUNDULIKA KUWA NI KARIBU ASLIMIA 20 YA WATU WALIOPIMA WALIKUTWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI AMBAYO YANAYOZIDI WASTANI WA KITAIFA WENYE WASTANI WA ASLIMIA 5.7.
AIDHA AMEFAFANUA KUWA SABABU KUBWA INAYOPELEKEA KUONGEZAKA KWA KASI MAAMBUKIZI HAYO NIKUTOKANA NA KUWAPO KWA WINGI WA WATU WANAOFIKA MAENEO HAYO KWAJILI YA SHUGHULIZO HIZO BILA KUWA NA FAMILIA ZAO HALI INAYOPELEKEA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA AMBAYO HUSABABISHA KUFANYA NGONO ZISIZO SALAMA.
HATA HIVYO BW. MWELEKA AMETOA WITO KWA JAMII HIYO KUBADILI TABIA NA KUWA WAAMINIFU KWA WAPENZI WAO ILI KUHAKIKISHA WANATOKOMEZA KABISA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI.

No comments: