Friday, November 2, 2012

POLISI YAWAKAMATA TENA VIONGOZI WA WAISLAMU

Story ya Rashid Mtagaluka, Dar es salaam


JESHI la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia viongozi wanne wa dini ya Kiislamu akiwemo Katibu Mkuu wa Bazara Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Maulana Ramadhani S
aid Sanze imefahamika.

Pamoja naye viongozi wengine waliokamatwa na jeshi hilo jana majira ya saa 5:00 za usiku huko Mbande nje kidogo ya jiji ni Sadik Gogo, Mukaddam Swaleh na mtu mwingine aliyefahamika kwa jina moja tu la Abdillah.

Habari za uhakika kutoka kwa viongozi wa Baraza hilo zimeeleza kuwa viongozi hao walikamatwa wakati walipokuwa wakitoka kumjulia hali mmoja wa viongozi wa BARAZA KUU anaishi Mbande.

Hata hivyo juhudi za kumpata Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam Solomon Kova ili aweze kuelezea ukweli wa taarifa hizo na makosa wanayotuhumiwa nayo hazikufanikiwa kwa kile kilichodaiwa ni sababu za kiusalama.

Wakati huohuo waislamu 49 waliofikishwa mbele ya Mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu wamegoma kuachiwa kwa dhamana hadi pale dhamana ya sheikh Ponda Issa Ponda itakapokuwa wazi.

Wakizungumza na mwandishi wetu leo asubuhi katika viunga vya mahakama hiyo, baadhi ya ndugu wa watuhumiwa hao wamesikitishwa na hatua ya mahakama kutoa dhamana kwa watuhumiwa wote isipokuwa mmoja wakati ambapo wote wanakabiliwa na shitaka moja.

wakasema hatua hioyo inaashiria ni jinsi gani nchi yetu inayoubiri utawala wa haki na sheria kinadharia zaidi kuliko vitendo.

Aidha taarifa zilizotufikia wakati tukenda mitamboni zineleza kuwa MAANDAMANO YA KESHO na ya amani yapo vilevile na yatafanyika nchi nzima huku kwa Dar es Salaam yakielekea ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni, na yale ya mikoani yataishia ofisi za wakuu wa mikoa

No comments: