Tuesday, November 6, 2012

LISU KUMSHITAKI RAIS BUNGENI

Story ya www.dankaijage.blogspot.com


MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema), ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni amesema kuwa anakusudia kupeleka hoja binasi bungeni kwa ajili ya kumshitaki  rais bungeni kutokana kufanya makusudi uvunjifu wa katiba ya nchi kwa kuteua majaji wasiokuwa na sifa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Lissu wakati akizungumza na waandishi wa habari hapa bungeni hii leo amesema kuwa anakusudia kufanya hivyo katika bunge la mwezi February mwaka ujao kutokana na Rais kuendelea kuvunja katiba ya nchi makusudi kwa kuwateua majaji wasiokuwa na sifa vinginevyo atengue uteuzi huo haraka iwezekanavyo.
 Alisema kuwa anakusudia kuwasilisha hoja ya kumsitaki raisi bungeni kwa kutumia kanuni za kudumu za bunge Sehemu ya 11 na Ibara ya 46A na 46B  ya katiba ya sasa kifungu cha 121,122,123,124,125 na 126 Azimio la kumwondoa rais madarakani.


Lissu amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini rais wan chi amekuwa kiongozi ambaye anavunja katiba ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa itendo cha kuwateua majaji ambao hawana sifa ya kuitwa majaji na wakati mwingine hata awajui hata jinsi ya kuandisha mienendo ya kesi kwa kiingereza na wapo majaji ambao wanaongezewa muda kwa kupewa mikataba jambo ambalo ni kinyume.
Amesema kuwa pamoja na kuendelea kuvunja katiba ya nchi lakini kuna malalamiko ya muda mrefu kutoka Ikulu tagangu mwaka 2008 lakini rais amekuwa akipuuzia na kuendelea kuwateua  majaji ambao wengine wanatuhumiwa kwa kutoa rushwa kwa mahakimu jambo ambalo alisema kuwa ni hatari kwa utoaji wa haki.
 “Rais anatakiwa kutengua uteuzi wa Majaji  mara moja kwani Majaji ambao wameteuliwa wameteuliwa kinyume na katiba ya sasa ya nchi na kufanya hivyo rais moja kwa moja anakuwa amevunja katiba ya nchi na njia pekee ni kupeleka hoja binafsi na watakapopatikana wabunge kati ya 71 hadi 73 ambao nia silimia na 20 ya wabunge wote raisi anaweza kuondolewa madarakani kutokana na maamuzi ya wabunge,” alisema
Aidha alisema kuwa hata kama bunge litashindwa kufanya maamuzi ya kumwondoa raisi madarakani kutokana na uvunjifu wa katiba kwa uteuzi wa majaji mbovu utaangaliwa utaratibu wa kumshitaki Rais katika vyombo vya sheria.
“itabidi tufanye hivyo hata kama tukishindwa lakini tutakuwa tumefanya kazi, najua kuwa wapo baadhi ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuvunja sheria na katiba kwa ajili ya kumlinda rais ambaye anavunja katiba ya nchi” alisema Lissu.
Kati ya majaji ambao Lissu aliwataja kuwa ni miongoni mwa majaji ambao wameteuliwa kwa kuvunja katiba ni pamoja na Mbarouk  Salim Mbarouk ambaye alisema kuwa ana vigezo vya kuwa jaji na kudai kuwa hana sifa ya kuwa jaji.

Lissu amesema kwa sasa jaji huyo ndo anasoma chuo kikuu hulia na hana hata shahada ya sheria jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa utendaji wa haki kwa wale ambao wanatakiwa kupata haki kutoka kwa majaji hao.
Kwa mujibu wa Lissu wapo majaji 2 ambao wanatuhumiwa na kutoa rushwa kwa mahakimu ili waweze kuwapitishia kesi zao na sasa ni majaji.
Mbali na hilo alisema kuwa kuna jambo jingine ambalo limebainika kuwa kuna jaji mkubwa nchini ambaye amegushi vyeti vyake na kujirudisha miaka nyuma na kumtaka aache mara moja mchezo huo.
“Kuna jaji mkubwa mno hapa nchini amegushi vyeti vyake ambaye alitakiwa kustaafu mwaka 2014 lakini kagushi vyeti vyake ili aweze kuonekana kuwa umri wake unamruhusu kustaafu mwaka 2017.
“Tunamtaka jaji huyo ambaye kwa sasa hatuko tayari kumtaja lakini iwapo ataendelea na msimamamo wake wa kugushi vyeti vyake kwa ajili ya kutaka astaafu mwaka 2017 badala ya 2014 tutantaja na tukimtaja hapatakalika” alisema Lissu.
Kwa hatua nyingine alimtaka Spika wa Bunge Anne Makinda kusoma Ripoti ya Tume ya ngwilizi ya tume maadili na kinga za bunge ambayo ilikuwa ikimchunguza na kumuhoji kwa madai kuwa alitoa kauli ya kuwadhalilisha Majaji na kudhalilisha muhimili wa mahakama kwa kile alichosema kuwa majaji wengi hawafai kwani hawana sifa.
Alisema kutokana na kauli yake ya Julai 13 mwaka huu ambayo aliitoa bungeni kwa wakati akiwasilisha hotuba yake kama Waziri kivuli wa Katiba na Sheri, Lissu aliwataja Majaji kuwa walioteuliwa na Rais hawana uwezo na sifa za kuwa majaji jambo ambalo lilimpelekea Spika kuunda kamati ya kumshitaki katika kamati ya Bunge ya maadili na kinga bungeni ili atoe maelezo na ushahidi kwa kauli hayke hiyo.
Kutokana na hali hiyo Lissu anadai kuwa kamati hiyo ilimuhiji na kumtaka atoe ushahidi jambo ambalo alilifanya na na kukamilisha ushahidi wa nyaraka mbalimbali na nyingine zikiwa zikitokea Ikulu ambazo zinamlalamikia Rais kwa kuvunja katiba kwa kuteua majaji ambao hawana sifa ya kuwa mamaji.
Alisema kutoka na hali hiyo Spika wa bunge anatakiwa kuwasilisha hoja hiyo ndani ya ukumbi wa bunge ili watanzania ambao wana wanafuatilia shughuli za bunge waweze kubainisha kuwa ni nani muongo na nani mkweli juu ya kauli hiyo.
“Wakati tupo katika kikao cha ndani cha wabunge wote 30 Ocktoba mwaka huu wabunge waliulizia kuhusu tume mbili zilizoundwa  ya kunichunguza dhidi ya kauli yangu hiyo na ile ya kuwacunguza wabunge kuhusiana na vitendo vya rushwa, lakini Spika alisema kuwa hiyo ni mali yake na atazipitia na anaweza kuzitoa akisha ziptia jamboa ambalo linaashiria kuzikalia ripoti hizo” alisema.
Alienda mbali zaidi na kudai kuwa ana uhakika wa kile alichokisema kuwa Majaji wanaoteuliwa na rais hawana sifa na ndiyo maana hakuna hata siku moja ambayo serikali ilisha wahi kukanusha taarifa hizo.
Alisema kuwa iwapo ripoti hiyo ambayo ilikuwa ikimchunguza ni wazi kuwa kutakuwa ni pata shika kwani Waziri wa Katiba na Sheria , Mathiasi Chikawe pamoja na Mwana sheria mkuu wa Serikali,Jaji Fredrick Werema watatakiwa kuwajibika.

No comments: