NENO LA BABA ASKOFU MKUU NORBERT MTENGA ......“hawa viongozi waliolitumikia taifa na kumwaga damu zaona jasho lao, na wamelipenda taifa la Mungu mpaka
kufa, na pengine wamedharauliwa na pengine kutokueleweka kwa sababu ya
kutumikia taifa lao, hawa wote sasa wafike kwa Mungu, wakutane na Julius
Nyerere na Kwa pamoja walitazame Taifa letu la Tanzania, tunawazika hawa wakati
taifa letu lina mazito kweli, lina mambo ya ajabu, mambo ya kutisha na mambo ya
hatari… TUFANYEJE… mkono wa Bwana utuangazie….”
<<<<<<>>>>>>>
STORY KWA KIFUPI
Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo la Shinyanga, Muashamu
baba Askofu Alyosius Balina, umeagwa rasmi leo jijini Mwanza katika kanisa la Epifania
Bugando,Jimbo kuu katoliki la Mwanza.
Mbele ya mamia ya waamini waliohudhuria katika Misa maalumu
kwa aajili ya kumuaga mtu huyu ambaye wengi wa waliosimama walimsifu kwa juhudi
za utendaji wake kiimani na katika taifa kwa ujumla, mkuu wa mkoa wa Mwanza
Eng. Evarist Ndikilo , amemtaja hayati Askofu Balina kama kiongozi hodari.
Askofu Balina , alikuwa maarufu kwa utetezi wake wa vikongwe
ambao wamekuwa wakiuawa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni wachawi, juhudi katika
kupambana na mauaji hayo ikiwa ni pamoja na mauaji ya walemavu wa ngozi, Askofu
Balina , alianzisha kituo cha redio kiitwacho FARAJA FM kilichopo mkoani
Shinyanga.
Hayati Askofu Balina , amefariki akiwa na umri wa miaka 67, alizaliwa 1945. Mazishi yake yatafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 10 Novemba.
RAHA YA MILELE UMPE EBWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE,... APUMZIKE KWA AMANI!!!!
STORY NA PICHA ZAIDI ZITAKUJIA KUPITIA
Kanisa la Epifania Bugando, hapa ndipo Misa takatifu ilipofanyika |
Watawa (Sister) hawa nao walijumuika kumuaga mjoli wao |
Jeneza lenye mwili wa Hayati Muasham Baba Askofu Aloysius Balina, hapa likiwa ndani ya kanisa la Epifania Bugando, mchana wa leo. |
Huu ndio mwili wa Marehemu Askofu Aloysius Balina, ni ndani ya Jeneza |
Mapadre waliohudhuria katika Misa hiyo |
Muasham Baba Askofu Thadeus Rwaichi, Jimbo kuu la Mwanza , aliongoza Misa hiyo |
Eng. Evarist Ndikilo, mkuu wa mkoa wa Mwanza, akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya serikali. |
“hawa viongozi waliolitumikia taifa na kumwaga damu zaona jasho lao, na wamelipenda taifa la Mungu mpaka
kufa, na pengine wamedharauliwa na pengine kutokueleweka kwa sababu ya
kutumikia taifa lao, hawa wote sasa wafike kwa Mungu, wakutane na Julius
Nyerere na Kwa pamoja walitazame Taifa letu la Tanzania, tunawazika hawa wakati
taifa letu lina mazito kweli, lina mambo ya ajabu, mambo ya kutisha na mambo ya
hatari… TUFANYEJE… mkono wa Bwana utuangazie….” HAYA NI MANENO YA ASKOFU MKUU, MWENYEKITI WA T.E.C, Muasham Baba Askofu Norbert Mtenga (Pichani)
No comments:
Post a Comment