Saturday, October 6, 2012

SERA YA MATIBABU KWA WAZEE NI POROJO


Story ya Ahmad Nandonde, imetumwa kutoka Moshi

SERA ya serikali kutoa huduma za matibabu bure kwa wazee imeshindwa kutekelezeka kwa vitendo na badala yake kubaki kama porojo katika maeneo baadhi hapa nchini ikiwemo wilaya ya Moshi.

Kwa uchunguzi uliofanywa na kituo hiki moja ya wilaya ya mkoa wa Kilimanjaro imeshindwa kutekeleza sera hiyo ambayo imeonekana kama ni kuwahadaa wazee hao.

Moja ya mzee Joseph Kimaro(72) kutoka katika kata ya Mwika kusini wilaya ya Moshi vijijini alisema kuwa huduma hizo za matibabu bure kwa wazee kwa upande wao bado imebaki kuwa kama kitendawili.

Iddy Muya(63)ambaye ni mwenyekiti wa wazee wilaya ya Moshi vijijini alisema tatizo la kutopatiwa matibabu kwa wazee sasa linaonekana kuwa ni jambo la kawida licha ya serikali kutaka wazee hao wapatiwe matibabu bure.

Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Ntumwa Mwako alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la kutopatiwa matibabu bure kwa wazee katika wilaya ya Moshi kwa kisingizio kuwa hospitali ya Wilaya bado haijakamilika.

Amesema wazee hao wamekuwa na wakati mgumu katika kupatiwa matibabu kutokana na hositali ya Himo kutokamilika lakini hata hivyo serikali ipo mbioni katika kuhakikisha njia mbadala inatumika katika kutatua tatizo hilo.

Tatizo linguine lililoonekana kuchangia huduma hii kusuasua ni pamoja na bohari kuu ya dawa (msd)kutotoa dawa kwa wakati  hali ambayo huwafanya wazee walio wengi kulazimika kujinunulia dawa pamoja na huduma nyingine.

No comments: