Monday, October 15, 2012

SAFARI YA MWISHO YA RPC BARLOW , MKOANI MWANZA HII HAPA

SIMANZI
Ikiwa inaandika historia ya afisa wa tatu  wa jeshi la polisi kuuawa mkoani Mwanza, hii ilikuwa shughuli ya kumuaga aliekuwa kamanda wa wa polisi mkoa wa mwanza ASCP Liberatus Barlow (53), akiwa ameacha mjane, na watoto wa nne.
Shughuli hii ilifanyika katika viwanja vya Nyamagana katikati ya jiji la Mwanza, ikihudhuriwa na mamia ya watu kutoka jiji hilo na viunga vyake , lakini pia watu kutoka mikoa ya jirani.
Viongozi wa kitaifa waliongozwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu , sera na uratibu wa bunge Ndg William Lukuvi, Upande wa polisi waliongozwa na Afande DCI Robert Manumba akimwakilisha IGP Saidi Mwema.
Shuguli ilianza majira ya saa Nne asubuhi hadi saa kumi jioni. BWANA AMETOA,  BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE..

Maafisa wa polisi , wakiuingiza uwanjani mwili wa Kamanda Barlow

Maafisa wa polisi wakiuweka sawa mwili wa Kamanda Barlow

Marehemu ASCP Barlow akiwa amelazwa  katika jeneza

Fr Anthony Manyanga , aliongoza Misa takatifu ya kumuaga Kamanda Barlow, hapa akitia ubani kulizunguka jeneza la Kamanda.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu  sera uratibu na bunge Wilium Lukuvi (katika) kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa mwanza Eng. Evarist Ndikilo, Kushoto ni DCI Robert Manumba


Waziri Lukuvi akiaga Mwili wa marehemu Barlow Leo hii . Picha na Migongo 1950 blog
Naibu waziri wa uchukuzi Eng. Charles Tzeba, akitoa heshima za mwisho kwa kamanda Barlow
Mjane wa marehemu Kamanda Barlow , hapa akitoa heshima za Mwisho mbele ya mwili wa marehemu mumewe.

No comments: