Saturday, October 6, 2012

MUSOMA WATAKA UWANJA UWANJA USIMAMIWE NA WIZARA

Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA.

WIZARA YA UCHUKUZI, IMETAKIWA KUSIMAMIA MRADI WA UJENZI WA UWANJA MPYA WA NDEGE ULIOPO WILAYANI SERENGETI MKOANI MARA, ILI KUWEZESHA WATALII WENGI KUTOKA NJE YA NCHI KUTEMBELEA MBUGA YA WANYAMA YA SERENGETI, NA HATIMAYE KUONGEZA PATO LA TAIFA.
KAULI HIYO IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA MARA, JOHN GABRIEL TUPPA, WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KWENYE UFUNGAJI WA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA HUO (RCC), KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA MJINI MUSOMA.
TUPPA AMESEMA WIZARA INAO WAJIBU WA KUSIMAMIA UJENZI WA UWANJA HUO, IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA MISINGI NA SERA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA KUHAKIKISHA UNAKIDHI MAHITAJI YOTE, ILI KUWEZESHA WATALII WENGI WA NDANI NA NJE YA NCHI KUTEMBELEA MBUGA YA WANYAMA YA SERENGETI.
KATIKA HATUA NYINGINE, TUPPA AMEELEZA KUSHANGAZWA NA KUSIKITISHWA NA MIPANGO FINYU DHIDI YA IDARA YA AFYA KATIKA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA HUDUMA YA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF), MKOANI HAPA, NA KWAMBA HUDUMA HIYO IMEDORORA ZAIDI HADI KUFIKIA ASILIMIA 0.6 YA MICHANGO YOTE.
AMESEMA KUKWAMA KWA MFUKO HUO KUNAUKOSESHA MKOA HUO KUPATA FEDHA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, HIVYO KUDUMAZA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI.

No comments: