Monday, October 29, 2012

MAAMBUKIZI YA UKIMWI MUSOMA YAMEKUA KWA ASILIMIA 3

Story ya AHMAD NANDONDE

MRATIBU WA TUME YA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI WA MKOA WA MARA EDWIN MWELEKA AMETOA TAKWIMU YA KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YA SASA MKOA WA MARA KUWA NI ASILIMIA 7.7% KUTOKANA NA UTAFITI ULIO FANYIKA MWAKA 2003 HADI 2004 AMBAPO KIWANGO CHA MAAMBUKIZI MKOANI HUMO KILIKUA ASILIMIA 3.5%.
AKIZUNGUMZA NA RADIO VICTORIA LEO OFISINI KWAKE AMESEMA KUWA KIWANGO CHA MAAMBUKIZI MKOA WA MARA KINA TOFAUTIANA TOKA WILAYA HADI WILAYA KWA KATI YA ASILIMIA NNE HADI 13.
AIDHA AMEZITAJA WILAYA ZENYE KIWANGO CHA MAAMBUKIZI NI RORYA (13%),MANISPAA YA MUSOMA MJINI (10%),MUSOMA VIJIJINI(6.4%),TARIME(6%),BUNDA(4.8%)NA SERENGETI NI ASILIMIA NNE.
HATA HIVYO AMESEMA KUWA VICHOCHEO VIKUU VINAVYOCHANGIA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU MKOANI MARA NI PAMOJA NA MWINGILIANO KATIKA MAENEO MBALIMBALI HASA KATIKA MAENEO YA WACHIMBAJI WA MADINI NA MIALO YA WAVUVI.
MWELEKA AMEONGEZA KUWA JAMII INAPASWA KUWA MAKINI KATIKA SWALA LA KUFANYA NGONO ILI KUEPUSHA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI MKOANI MARA HASA VIJANA KWANI NDIO NGUVU KAZI YA KESHO NA TAIFA KWA UJUMLA

No comments: