Tuesday, September 4, 2012

WAZIRI LWENGE AANZA ZIARA MKOANI MTWARA LEO HII

Imeandikwa na Idrsia Bandali , akiwa Masasi.

Naibu waziri wa wizara ya miundombinu na ujenzi Waziri wa Ujenzi Ndugu Gerson Lwenge leo anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani mtwara.

Ndugu Lwenge anaanza ziara hiyo akitokea mkoani Ruvuma, ambapo baada ya kupokelewa atatembelea katika daraja linalounganisha Nchi za Tanzania na Msumbiji darja la mkapa(,mtambaswala)


Pamoja na kutemnbelea daraja hilo Ndugu Lwenge pia anatarajia kukagua miundo mbinu mbalimbali ya barabara pamoja na ujenzi wa daraja na Nagoo unaondelea hivi sasa


Aidha Ndugu Lwenge anatarajia kufanya ziara katika wilaya zote zilizopo mkoani mtwara ili kujionea kasi ya ujenzi wa miundo mbinu inayosimamiwa na wizara yake.


Ziara ya Ndugu lwenge inataraji kubai miradi ambayo inasimamiwa na wizara yake kwa ile iliyokamilika na mabayo bado haijakamilika

No comments: