Monday, July 16, 2012

TAMPRO YAMTUNUKU WAZIRI HAWA GHASIA TUZO YA MWANAMKE BORA KWA UVAAJI WA STARA (HIJAAB)

Imeandikwa na Rashid Mtagaluka

JUMUIYA ya wanataaluma wa Kiislamu nchini TAMPRO, jana ilimtunuku Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Abdurhamani Ghasia (MB) tuzo kwa niaba ya wanawake wanaojisitiri na kudumisha vazi la Hijaab nchini kwa mwaka 2012/2013.
Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Karemjee jijini Dar es Salaam wakati wa hitimisho la kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililoandaliwa na TAMPRO wakishirikiana na Amana Bank.

Mbali na Waziri Ghasia, watu wengine waliobahatika kutunukiwa tuzo ni pamoja na shekh Ponda Issa Ponda, aliyekabidhiwa tuzo kwa niaba ya wanaharakati wote nchini.

Kondo Juma Bungo naye alikuwa miongoni mwa waliotunukiwa tuzo kwa mchango mkubwa aliokuwa ameutoa kwa taasisi hiyo juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na dindi ya Kiislamu.

PICHA MBALI MBALI ZA HAWA GHASIA KATIKA VAZI HILO, HIJAABNo comments: