Thursday, July 5, 2012

MSIMAMO TOFAUTI NA BAKWATA HUU HAPA.... NI KUHUSU SENSA... 2012

Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hayatul Ulamaa), umedai Waislamu hawatashiriki sensa hadi kipengele cha dini kiwekwe katika dodoso la sensa na usimamizi wake uwe wa uwiano baina ya dini zote.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, wanazuoni hao walisema msimamo wao wa kutoshiriki sensa upo palepale kama walivyokubaliana na mashekhe wa jumuiya na taasisi zote za Kiislamu Tanzania waliohudhuria mkutano wa viongozi wa dini kuhusu sensa uliofanyika Dodoma Juni 11.

Akisoma tamko hilo, Mjumbe wa Kamati Kuu, Ally Basaleh alisema katika mkutano huo mashekhe wote waliohudhuria waliweka msimamo kuwa Waislamu wasishiriki sensa mpaka kipengele cha dini katika dodoso la sensa kitakapoingizwa.

"Hay-at inataka ieleweke si kwamba Waislamu wanapinga sensa au hawaelewi umuhimu wake, bali kwa kweli Waislamu wanaichukulia Sensa ya Watu na Makazi katika mambo yanayoendana na Sunnah,” alisema Basaleh.

Alisema hata Mtume Muhammad (S.A.W) alipohamia Madinna, aliagiza ifanywe hesabu ya idadi ya wakazi wote wa Madinna kwa mujibu wa makundi ya jamii yao kwa lengo la kuwajua na hivyo kuwapatia huduma za kijamii zinazohitajika.

Source: http://www.wavuti.com na Habari leo

1 comment:

Vedasto F.Ndibalema said...

Naamini hao viongozi wa bakwata ndio wanaowachanganya waislam tz, kwani watu wanakubalia hivi wao wanageuka