Wednesday, June 20, 2012

PICHA ZA JOHN MNYIKA BAADA YA KUTOLEWA BUNGENI JANA

Picture

 Askari wa bunge wakimsindikiza kutoka nje ya ukumbi

Picture

KAULI YENYEWE HII HAPA
‘...tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa sababu ya wabunge na bunge, na tumefika hapa tulipo kwa sababu ya upuuzi wa CCM..."

BAADAE AKASEMA HAYA....
"...... kusema ni udhaifu si matusi...ni ukweli unaohitaji kutafakariwa tu kwa kweli...kwa mujibu wa katiba yetu mwenye mamlaka makubwa juu ya uendeshaji wa shughuli za serikali ni raisi wa nchi...na mwenye mamlaka juu ya bajeti ni rais wa nchi ukiangalia mfano ibara ya 99 ya katiba inakataza baadhi ya mambo bunge haliwezi kuyashughulikia...mfano masuala yanayohusu kuongeza kodi na mengineyo tumekuwa tukipiga kelele kwamba tunataka kupanua wigo wa vyanzo vya mapato...na serikali haijatekleza.... kitendo cha rais kutokuleta mapendekezo ni udhaifu wa taasisi ya urais...kuna ibara ya 90 ya katiba yetu vilevile inatamka ..inampa mamlaka rais ya kulivunja bunge pale bunge linapoikataa bajeti ya serikali... tafsiri yake ni kwamba bunge letu halina mamlaka makubwa juu ya bajeti..."
CHANZO MAHOJIANO NA VOA
KUHUSU TAMKO LAKE RASMI
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.

Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.

Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge.

Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika
19 Juni 2012

No comments: