Monday, June 11, 2012

KESHO KIKAO CHA BUNGE KUJADILI BAJETI 2012/2013, KINAANZA ....HEBU TUTAFAKARI HAYA

WAZIRI wa fedha Mustafa Mkulo mwaka jana alitaja vipaumbele 12 katika utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012.
Vipaumbele vya waziri Mkulo ni kilimo/mifugo/uvuvi; elimu; nishati; miundombinu; maendeleo ya viwanda; afya; maji; ardhi/nyumba/makazi; raslimali watu; sayansi/ teknolojia; huduma ya fedha na masuala mtambuka.
Suala hapa ni je.... lipi limefanikiwa kwa kiwango gani
KWA MUJIBU WA MKULO 2011/2012 SERIKALI ILIKUSUDIA HAYA:-
2.2. Serikali inataka kufanikisha nini katika mwaka 2011/2012 
Kwa ujumla, Bajeti hii imelenga kuchukua hatua za kupunguza gharama za maisha kwa  
wananchi na  kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kutekeleza yafuatayo:-  
A. Kuongeza ubora wa huduma za Afya na Elimu  nchini kupitia:  
• Kudumisha faida na mafanikio yaliyopatikana katika  sekta ya afya na elimu 
kuboresha upatikanaji wa huduma bora zinazotolewa na sekta hizi.  
B. Kuboresha tija katika  uzalishaji wa mazao ya Kilimo na mfumo wa Umwagiliaji 
kupitia: 
• Kuhamasisha uwekezaji wa  sekta binafsi  katika Kilimo, • Kuimarisha Utafiti na kukuza /kuendeleza uzalishaji katika kilimo na tekinolojiia za matumizi ya mashine katika kilimo, • Kuboresha  miundombinu iliyopo ya hifadhi ya taifa  ya chakula na kuanzisha vituo vingine katika maeneo muhimu, • Kujenga vituo muhimu vya kuhifadhia maji (yaani; mabwawa madogo, ya kati na makubwa), umwagiliaji na miundombinu ya kupitisha maji kwa ajili ya skimu 33, • Kukarabati skimu za umwagiliaji za asili zilizopo,  na vyama vya msingi vya ushirika. na • Kuendeleza na kuimarisha mashirika ya Umma.
MGAWANYO

 Mgawanyo wa kisekta kama asilimia ya bajeti nzima   
Elimu, 16.9, Miundombinu,20.6, Afya, 8.9, Maji, 4.6, Kilimo, 6.8, Nishati &Madini, 4 na Mengineyo, 38.3
UCHAMBUZI WA ZITTO KABWE (WAZIRI KIVULI WA WIZARA HUSIKA) MWAKA HUU 2012/2013(kwenye wordpress)
Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;
1    Huduma kwa Deni la Taifa          Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2    Wizara ya Ujenzi.                          Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3    Wizara ya Ulinzi                          Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4    Wizara ya Elimu                              Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5    Wizara ya Nishati na Madini    Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
 TOTAL                                        TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
KWA MUJIBU WA ZITTO KABWE

Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la  Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma.
Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.

No comments: