Wednesday, June 27, 2012

ALIYOYASEMA BUNGENI , MBUNGE ZITTO KABWE HII LEO


Wenye Mabilioni Uswisi(Switzerland)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Waziri Mkuu kumekuwa na taarifa ambazo 
zimeandikwa katika vyombo vya habari toka wiki iliyopita. Lilianza Gazeti la The East African baadaye wakaja Gazeti la The Citizen na leo nimesikia kwamba Gazeti la Mwananchi limezungumza kwamba kuna Watanzania 6 wana fedha katika akaunti kule Uswisi zaidi ya shilingi bilioni 303. India walipopata taarifa hizi kutoka Benki ya Uswisi waliwataja majina watu wote wana siasa na wafanyabiashara wenye fedha nje na fedh zile zikachunguzwa zile ambazo zimepatikana kwa haramu zikarejeshwa India. Nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu uagize TAKUKURU na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwanza tutambue ni Watanzania gani hawa na fedha hizi zimepatikana kwa njia zipi na zile ambazo zimepatikana kwa njia ya wizi na ufisadi zirejeshwe nchini mara moja. Kwa sababu hatujaanza kunyonya utajiri huu wa gesi tayari kuna watu ambao wameshaanza kutajirika nao.
Tutakapoanza kunyonya hali itakuwaje? Kwa hiyo, nilikuwa naomba suala hili Serikali ilichukulie kwa uzito mkubwa ili itume salaam kwa mtu yeyote ambaye anatarajia kwamba atafaidika na utajiri wa rasilimali ya nchi kama gesi na madini na kadhalika ajue kwamba kokote atakapoficha fedha zake tutazifuata na zitarudi katika nchi hii. Nilikuwa naomba Waziri Mkuu aweze kuliangalia jambo hili kwa ukaribu sana.
Zuia Makampuni ya Kigeni kwenye Ulinzi
Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu hivi sasa Kiongozi wa Upinzania amezungumza jana kuna meli ziko Pwani ya Mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara zinatafuta mafuta. Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuna kampuni hata moja ya mafuta inayonunua hata mchicha kutoka Tanzania. Meli zote ambazo ziko Bandari Mtwara zinakwenda kupeleka huduma kwenye maeneo ambayo yanatafuta mafuta yanapata mchele, nyanya, vitunguu, mchicha, mafuta ya kula na kadhalika kutokea Kenya kwa sababu hatujaweka utaratibu wa kufanya nchi yetu iweze kufaidika na utaraji huu mwanzoni. Kwa sababu hatua hizi za mwanzoni hakuna kodi ambayo tunapata kwa sababu mafuta bado yanatafutwa.
Hatua hizi za mwanzoni tunatakiwa tufaidike na fedha inayokuja, watu waweze kutumia fedha za kutoka ndani. Lakini hali ilivyo hivi sasa ni kwamba makampuni ya mafuta yanatumia zaidi ya dola milioni 161 kwa ajili ya shughuli za ulinzi na makampuni yanayolinda, ni makampuni ya nje. Yanabeba silaha kubwa kubwa, siku yakiamua kutugeuka na Navy yetu ilivyo tutapata shida. Nilikuwa naomba tutenge resources za kutosha na hata kama hatujaziweka kwenye bajeti sasa hivi, tuangalie, tuimarishe Navy na tupige marufuku, tuandike sheria kabisa kwamba itakuwa ni marufuku kwa raia yeyote wa kigeni kubeba silaha zozote kubwa ili kuweza kuhakikisha kwamba ulinzi ama unafanywa na watu wa ndani au unafanywa na Navy yetu tuweze kulinda mipaka yetu vizuri.
Utafutaji Mafuta Zanzibar Uendelee
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuna suala ambalo halijaisha na Kiongozi wa Upinzani Bungeni jana amelizungumzia la mafuta na gesi katika masuala ya muungano. Nilikuwa naomba jambo hili tulimalize kwa haraka. tulimalize kwa haraka na mimi sioni ubaya kwa kweli, sioni ubaya hata kidogo kama tukiamua kwamba shughuli zote commercial not upstream, sio masuala ya regulation, sio masuala ya vibali, sio masuala ya kutoa leseni, masuala yote commercial yanayohusiana na mafuta na gesi, kila upande wa muungano ushughulike na masuala yake.
Hakuna sababu ya kunga’gania jambo hili kama sisi tuna dhahabu, tuna tanzanite, tuna madini hayapo sehemu ya muungano, kwa nini mafuta na gesi yawe sehemu ya muungano? Hili ni jambo ambalo tulimalize, liishe tuimalize hii kero, vikao na vikao havitasaidia, tuimalize hii kero, tu-move forward watu wa Zanzibar waanze utaratibu wao wa kufanya utafutaji wao, waangalie kama watayapata hayo mafuta au hawatayapata, sisi tayari huku Bara tumeshapata, tuna matrilioni ya gesi, basin a wenyewe tuwaache waendelee na utaratibu wao. Hakuna sababu ya kuchelewesha jambo hili tuweze kulimaliza mapema.
TZS 40 Bilioni kwa Kiwira
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni suala la Kiwira na baadae nitakuwa na mazungumzo na baadhi ya Mawaziri kuhusiana na suala hili tuliangalie kwa makini. Tumetenga shilingi bilioni 40 kwenye fedha ya maendeleo Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nini? Kuna fedha ambayo tunaenda kuwalipa watu ambao wameuharibu mgodi. Kwa nini tulipe watu ambao wameuharibu mgodi?
Lakini tunaenda kulipa bilioni 40 sio kwa Kiwira nzima..
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. 

No comments: