Monday, May 14, 2012

TAFAKARI YA WANASHERIA JUU YA VIAPO VYA WABUNGE..... WEWEMsomaji wetu UNAMTAZAMO GANI

BAADHI ya wanasheria wamesema utata ulioibuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwateua wabunge na kuwaapisha kuwa mawaziri kabla ya kuapa ubunge, ni matokeo ya ubovu wa katiba iliyopo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanasheria hao wamesema ni vigumu kusema Rais alivunja Katiba au la katika uteuzi huo kwani ipo kimya katika hilo.

Wataalamu hao wameiomba jamii kutumia fursa iliyopo ya kutoa maoni kuhusu marekebisho ya Katiba kuangalia kasoro hiyo na kuirekebisha. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla amesema katiba haisemi kama hatua hiyo ya Rais ni uvunjaji wa katiba ama la.

“Katiba yetu haimkatazi wala kumruhusu Rais kuwaapisha mawaziri aliowateua ambao hawajaapa kuwa wabunge,” alisema Stolla. Alisema Ibara ya 56 ya Katiba inaeleza kuwa Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

”Hapa kwenye kiapo kingine chochote, ndiyo tunapozungumzia kiapo cha Bunge,” alisema Stolla. Alisema kutokana na hali hiyo ni vigumu kueleza kwa uhakika kwamba Rais amevunja Katiba au la kwa kuwa ipo kimya. Mwanasheria mwingine, Harold Sungusia alisema Rais hajavunja Katiba na utata huo umetokana na ubovu wa katiba iliyopo.

“Ibara ya 56 haijatengamaa. Sheria inayosimamia viapo vingine vyovyote… Inasema waziri ataapa viapo viwili, kiapo cha uaminifu… lakini kifungu cha 15 cha hiyo sheria kimeeleza kuwa kinachofanywa na waziri hata kama hajaapishwa siyo batili,” alisema Sungusia. Alichofanya Rais kina utata kwa kuwa kuna makundi mawili ambayo yanafikiria tofauti; wale wanaosema Katiba ni mbovu na wale wanaosema kuwa ameivunja.

“Kama Katiba ni sheria iliyotungwa na Bunge, Rais Kikwete atakuwa amevunja katiba lakini kama haijatungwa na Bunge basi hajavunja Katiba,” alisema Sungusia na kuongeza:

(Mwananchi Jmosi 12 may)

No comments: