Monday, May 7, 2012

HOLLANDE AMBWAGA SARKOZY .. KATIKA DURU YA PILI YA UCHAGUZI


Francois HollandHabari za awali zinaonesha kuwa mgombea urais wa Ufaransa wa chama cha kisoshalisti, Francois Hollande, amemshinda rais wa sasa, Nicolas Sarkozy, kwa asili-mia-3 hadi 5.

Bwana Hollande anakuwa rais wa kwanza wa kisoshalisti nchini Ufaransa, kwa kipindi cha miaka 17; na atakuwa wa kwanza kumshinda rais aliyetumika kwa muhula mmoja tu, tangu mwaka wa 1981.


Huku Wasoshalisti wanasema kazi ya mwanzo ni kufanya majadiliano tena, juu ya sera za kiuchumi za Umoja wa Ulaya.

Rais Sarkozy alikiri kuwa ameshindwa, na alimpigia simu Bwana Hollande kumtakia heri,Punde baada ya kura za awali kuonesha matokeo.

Vyanzo vingine vya habari vinadai kuwa Hollande ni Msoshalisti wa pili kushikilia nafasi ya urais , tangu uchaguzi wa moja kwa moja mwaka 1958.

(BBC na RFI)

No comments: