Sunday, May 13, 2012

ALICHOKISEMA RAIS WA SAUTSO - SAUT- MWANZA KUHUS BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

KAULI YANGU KUHUSU UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI.


Jana nimetangaza baraza la mawaziri lenye jumla ya wizara 15. Mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu wa wizara walioteuliwa wamekidhi vigezo na sifa zilizotakikana.

Uwezo wa kifikra, umakini, utii, utendaji, na uaminifu ndio sifa zilizotumika kuteua baraza la mawaziri. Ni vema ikaeleweka kuwa waziri si bora kuliko naibu wake au katibu mkuu wa ...wizara. Wote ni wateule wa rais, wenye lengo moja kuhakikisha ilani ya uchaguzi inatekelezeka kwa ufanisi.

Aidha hakuna aliyeteuliwa kwa urafiki, ukabila, udini au namna alivyosaidia kufanikisha kampeni. Vilevile hakuna mtu aliyeachwa kwa sababu tu ya kabila lake, dini yake au urafiki wake na rais. Vigezo hivyo haviwezi kukupa au kukunyima nafasi ya uongozi. Hivyo kabla hujampima mtu kwa darasa analotoka, pima kwanza uwezo wake. Huenda anatoka darasa moja na rais, lakini hicho si kigezo kilichotumika kumpa nafasi, bali uwezo wake.

Mwisho nitumie fursa hi4 kuwapongeza wote waliopata nafasi ya kuwa ndani ya baraza. Nawatakia utendaji mzuri wenye mafanikio, ili kuhakikisha serikali hii inakuwa alama ya mabadiliko ya kweli hapa SAUT. Ni muhimu pia kuwakumbusha kuwa uwaziri hauna mkataba, hivyo kila afanye kazi kwa tahadhari maana sintasita kumchukulia hatua yeyote atakayekwamisha azma yetu ya kufikia mabadiliko ya kweli. Pia nawapongeza zaidi wote walio nje ya baraza maana wana nafasi nzuri ya kukosoa, kushauri, na kutoa maoni kuhusu utendaji wa serikali maana waswahili husema aliye nje ya uwanja huona mchezo vizuri kuliko aliye ndani. Nawatakia mafanikio ktk utendaji wenye ufanisi. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SAUT!

No comments: