Sunday, April 29, 2012

ALICHOKIANDIKA KWENYE FACEBOOK...RAIS MTEULE WA SAUTSO...SAUT MWANZA


Malisa Godlisten E.J


Nawashukuru ndugu zangu wa SAUT kwa imani kubwa mliyoonesha na kunipa ushindi wa 70%. Naahidi kuwatumikia kwa bidii na maarifa.

Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kuunda baraza la mawaziri ambalo litakuwa kiungo muhimu kati ya wanafunzi, uongozi wa chuo, na asasi nyingine za ndani na nje ya chuo. Naomba tutoe ushirikiano kwa wale watakaochaguliwa.

Nawashukuru wote walionipigia kura. Lakini ni vema... ikaeleweka baraza la mawaziri litakuwa dogo lenye ufanisi na tija. Uteuzi utazingatia uwezo wa mtu, na si namna mtu alivyojitolea kwenye kampeni. Wale ambao hawatapata nafasi ni muhimu wakaheshimu maamuzi ya wale waliopata nafasi. Na wale watakaopata nafasi waheshimu mawazo na maoni ya waliokosa nafasi. Tushikiane ili kuweza kutengeneza serikali makini.!

No comments: