Thursday, March 22, 2012

WIKI YA MAJI VIWANJA VYA SAMORA IRINGA : JK ASEMA WANASIASA WAACHE SIASA KWENYE VYANZO VYA MAJI


Rais Kikwete akikagua mradi wa maji wa Itunundu Pawaga wilaya ya Iringa
 RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa maombi ya wananchi wa Ihefu Mbarali ambao wanaomba kurudi katika eneo la Ihefu hayatatekelezwa kamwe na serikali yake kutokana na umhimu wa eneo hilo kwa Taifa.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji Kitaifa yaliyofanyika mkoani Iringa katika uwanja wa Samora, mjini Iringa

Rais amesema kuwa ni vema viongozi wa serikali na wale wa kisiasa kuendelea kutoa maamuzi magumu kwa wale wanaotaka kuharibu vyanzo vya maji nchini badala ya kuwaonea huruma wananchi hao wanaotaka kuharibu vyanzo vya maji. Na kuonya wanasiasa nchini Kuacha tabia ya kuwatetea wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi za Taifa kwa ajili ya kupata mtaji wa kisiasa .

Amesema kuwa baadhi ya mito hapa nchini imeendelea kuathirika kutokana na muingiliano wa shughuli za binadamu
Na kwamba mito mingi ukiwemo mto Ruaha, maji yake yameendelea kupungua kwa kasi na kuwa tayari ametoa maagizo kwa wizara ya maji ,wizara ya Maliasili na utalii pamoja mikoa inayozunguka mto huo kukutana siku moja kwa ajili ya kuunusuru mto Ruaha unaoendelea kukauka .

Kuhusu hali ya mvua … amesema kuwa hali ya mvua kwa sasa bado ya wasiwasi na ni vigumu kutabiri hali hiyo kutokana na mvua kunyesha tofauti na zamani ambapo mvua zilikuwa zikijulikana zinaanza lini na kumalizika wakati gani.


Kutokana na mabadiliko hayo rais amesema kuwa watanzania hwana budi kutumia teknolojia ya kisasa ya kilimo kwa kutumia umwagiliaji wa mat one Kama njia ya kupunguza kasi ya matumizi ya maji.

Amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji wa matone na mkakati wa wananchi kuanza kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji badala ya kutegemea mito zaidi , kutayafanya mazingira kuwa endelevu… na kuhimiza wananchi kutunza mazingira pamoja kulinda na kuhifadhi vyanzo hivyo vya maji .

Kuhusu tatizo la maji nchini Rais kikwete

Amesema kuwa serikali imejipanga kupunguza kwa kasi tatizo la maji nchini kwa kuanza na miji 19 nchini na kuwa malengo ya kufikisha huduma hiyo ya maji yameendelea kutekelezwa vyema… na kuwa lengo ni kufikisha asilimia 65 katika vijiji ifikapo mwaka 2015

Hata hivyo alipongeza jitihada za wadau mbali mbali wakiwemo wahisani ambao wamendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza miradi ya maji ikiwemo benki ya dunia na kwamba fedha za maji katika miji mbali mbali nchini tayari zimepatikana na kuwa kinachosubiriwa sasa ni kuanza kwa kazi hiyo .

No comments: