Friday, March 23, 2012

WIKI YA MAJI IRINGA : VIONGOZI WAPOTEZANA NA MSAFARA WA RAIS

Magari yaliyopotea kwenda Ikulu yakiwa uwanja wa Ndege Nduli

Wiki ya maji yamalizika kwa kituko cha mwaka mkoani Iringa baada ya viongozi waliokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete kupotea mjini Iringa.

Tukio hilo limetokea majira ya 9.30 alasiri baada ya viongozi hao kutoka katika chakula cha mchana na Rais Kikwete katika ukumbi wa St Dominic ulipo eneo la RETCO kata ya Gangilonga.

Viongozi hao wakiwemo viongozi wa Manispaa ya Iringa pamoja na wale wa kitaifa waliofika katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa ,Sherehe zilizofanyika mkoani Iringa walijikuta wakipotea badala ya kuelekea Ikulu wao walielekea uwanja wa Ndege Nduli nankulazimika kugeuza .

Mbali ya viongozi hao kupotea pia askari polisi wa FFU na wanahabari waliokuwemo msafara huo nao walijikuta wakipotezwa na viongozi hao baada ya kuelekea uwanja wa Ndege Nduli na kugeuza eneo la FM Abri na kuelekea Ikulu.

Mmoja kati ya viongozi waliokuwemo katika msafara huo alisema kuwa kupotezana kwa viongozi hao katika msafara huo ni kutokana na magari kugawanyika kwa yale ya Manispaa ya Iringa kuelekea uwanja wa Nduli na msafara wa Kikwete kuelekea Ikulu na askari aliyekuwepo eneo hilo kushindwa kujua magari yanayokwenda Ikulu ni yapi na yanayokwenda uwanja wa Ndege kabla ya Rais ni yapi.Kwa mujibu wa blog ya Mzee wa matukio (Francis Godwin)

No comments: