Wednesday, March 21, 2012

MACINI WA MAN CITY ATAKA WACHEZAJI WAPIMWE ZAIDI -- NI KUFUATIA MUAMBA KUANGUKA NA KUZIMIA


Roberto Mancini

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema wachezaji wa Ligi Kuu hawana budi wapimwe afya zao mara mbili kwa mwaka.

Roberto Mancini asisitiza uchunguzi zaidi wa afya za wachezaji
Taarifa zinazohusianaKandanda, MichezoMancini anahisi utaratibu wa upimaji wa sasa "hauna uhakika" sana.
"Wakati nilipoangalia utaratibu wetu wa matibabu miaka miwili iliyopita, niliingiwa na hofu. Nilisema tunahitaji kufanya zaidi ya hapa," alisema.

Mancini ametoa maoni yake baada ya Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu Richard Scudamore kusema kutakuwa na utaratibu wa kupitia masuala ya upimaji baada ya Fabrice Muamba kuanguka na kuzirai kutokana na matatizo ya moyo.

KATIKA HATUA NYINGINE..

Fabrice Muamba sasa anaweza kutambua familia na jamaa zake na hata kuweza kujibu maswali. Hii ni kwa mujibu wa wakuu wa kilabu yake Bolton Wonderers pamoja na madaktari.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, pia anaweza kupumua bila usadizi wa mashine , lakini hali yake ingali mbaya kiasi cha kusalia katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Mwamba alianguka uwanjani na kuzimia mnamo Jumamosi wakati wa mechi kati ya klabu hiyo na Spurs.

Moyo wake Ulisimama kwa masaa mawili lakini tangu hapo ameanza kuonyesha dalili za kuimarika kiafya.
Madaktari wamesisitiza kuwa hali ya Muamba sio mahututi lakini ni mbaya.


No comments: