Sunday, March 25, 2012

KWA WALE WENYE TV ZA VICHOGO TZ.. MWISHO WAJA ....

TANGAZO LA USITISHWAJI WA MATANGAZO YA TELEVISHENI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA ANALOJIA NA KUHAMIA TEKNOLOJIA YA UTANGAZAJI YA DIJITALI NCHI


Nchi yetu itasitisha rasmi matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia na kuhamia teknolojia ya dijitali ifikapo tarehe 31 Desemba, 2012 saa sita usiku.

Lengo la kufanya hivyo ni kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano duniani kote. Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya dijitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo ya televisheni, ongezeko la chaneli za televisheni litakalotokana na matumizi bora ya masafa, kuwepo kwa masafa ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwamitambo ya analojia inayotumia masafa mengi, kuongezeka kwa watoa huduma wa mawasiliano ya simu, matangazo ya televisheni kupatikana katika vifaa vingi zaidi vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti.

Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha na kuwahimiza wananchi wote kufanya maandalizi ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kutumia ving’amuzi vitakavyowezesha televisheni za analojia zinazotumika kwa sasa kupokea matangazo ya dijitali au kutumia televisheni zadijitali ambazo hupokea matangazo ya digitali moja kwa moja.

Kwa taarifa zaidi piga simu namba 0784 558 271 au tembelea tovuti zifuatazo:wwww.mst.go.tz au http://www.tcra.go.tz/

No comments: