Tuesday, August 9, 2011

BREAKING NEWSS:

Suala la upatikanaji na uuzwaji wa mafuta hapa nchini limechukua sura mpya hii leo baada ya kuombewa mwongozo wa spika bungeni na mbunge wa bumbuli Januari Makamba, ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia nishati na madini, kwa kusema kuwa ni muhimu bunge likajadili suala hili kama jambo la dharura na kupata ufumbuzi wa suala hilo hii leo.
Kauli hiyo ilimlazimu naibu spika wa bunge kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya uongozi wa bunge kujadili kusitisha shughuli za bunge ili kujadili suala hilo ambalo limeanza kutishia uchumi wa taifa.
Jijini Dar es salaam na mtwara jana na leo bado kumekuwa na misururu ya watu wakisubiri huduma hiyo huku baadhi ya vituo vikiwa vimesitisha utoaji wa huduma .
Wiki iliyopita Ewura ilitangaza bei elekezi mpya za nishati, ambapo petroli itauzwa kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asimilia 9.17, dizeli kwa Sh 173.49 ambayo ni sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa kwa 181.37, sawa na asilimia 8.70.

No comments: