Friday, April 22, 2011

JK apongezwa kwa kutekeleza ahadi kwa vitendo
Na Idrisa Bandari
Mtwara
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa mtwara umetoa pongezi kwa mwenyekiti wa chama hicho taifa ndugu jakaya mrisho kikwete kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa mkoani Dodoma katika maadhimisho ya kutimizwa kwa miaka 34 ya chama cha mapinduzi.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa ambaye Pia ni Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Mtwara Ndg, Aroon Ngazagu alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Katika Makao makuu ya chama hicho Mkoani humo.
Bw.Ngazagu ametoa pongezi pia kwa Serikali kwa kukubali kuondoa muswaada uliopelekwa Bungeni kwa hati ya dharura kwa ajili ya uundaji wa tume itayo ratibu mchakato wa kukusanya maoni juu ya uundaji wa katiba mpya.
Chama cha Mapinduzi hivi karibuni kimefanya mabadiliko kwa kuwachagua wajumbe wa Sekretarieti na kamati kuu ya Chama hicho.

No comments: