Tuesday, September 26, 2023
UFARANSA YAKUBALI YAISHE KWA NIGER
Hatimaye, baada ya wiki kadha za vuta nikuvute, Ufaransa imesalimu amri mbele ya
takwa la Niger na kutangaza kwamba, balozi wa Ufaransa nchini Niger, Sylvian
Itte, atarejea Paris katika saa chache zijazo. Tangazo la Ufaransa linasema pia
kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo nao wataondoka Niger ifikapo mwishoni wa mwaka huu.
Sambamba na kutangazwa kwa habari hii, Baraza la Kijeshi la Niger katika taarifa
yake limeeleza kuwa, kuondolewa kwa wanajeshi wa Ufaransa na balozi wa Ufaransa
nchini Niger ni wakati wa kihistoria kwa nchi hiyo na kutangaza katika taarifa
yake kwamba leo tunaadhimisha enzi mpya katika njia ya uhuru na mamlaka ya
kujitawala Niger. CHANZO: PARSTODAY
Monday, June 5, 2023
HAKUNA VISA KUINGIA NCHI YA AFRIKA MASHARIKI
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuondoa gharama ya viza baina yao.
Taarifa zaidi zinasema, gharama ya viza imeondolewa kwa watu wanaotaka kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya jumuiya hiyo kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara.
Lengo la uamuzi huo limeelezwa kuwa ni kukuza mahusiano miongoni mwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa nchi husika.
Kuondolewa kwa gharama ya viza ni sehemu ya vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs) vilivyoondolewa na jumuiya hiyo, huku vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa, na vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo. CHANZO#parstoday
VURUGU ZAENDELEA NCHINI SENEGAL, HUDUMA YA INTERNET IMEKATWA
Serikali ya Senegal imepunguza ufikiaji wa huduma za intaneti na simu za mkononi katika baadhi ya maeneo kwa sababu ya ghasia mbaya ambapo jumbe za "chuki na uasi" zimetumwa mtandaoni.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekumbwa na maandamano na ghasia kwa muda wa siku tatu ambapo ambapo watu 16 wameuawa. Ghasia hizo ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
Wiki iliyopita, serikali ilizuia upatikanaji wa baadhi majukwaa ya mitandao, lakini watu wengi waliweza kujipenyeza katika mitandao iliyofungwa kwa kutumia mfumo wa VPN ambao huficha eneo la mtumiaji. CHANZO#parstoday
Sunday, March 13, 2016
Sunday, August 30, 2015
MSIKILIZE MAMA HELEN KIJO BISIMBA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KATIKA SIASA
MAELEZO KWA UFUPI...
MSIKILIZE MAMA BISIMBA , NILIPOZUNGUMZA NAE KUHUSU HILI
Utumishi wa umma katika nchi yetu
unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za
Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake.
Kanuni za kudumu za utumishi toleo la 1994 , kifungu Na. A.1 (66) Kinatafsiri
mtumishi wa umma kama mtu yoyote anayeshikilia ofisi ya umma ambayo imepewa
mamlaka ama inatekeleza wajibu wenye asili ya umma, iwe chini ya utawala wa
moja kwa moja wa Rais au la. Na inajumuisha maofisa walio chini ya Serikali za
Mitaa ama Mashirika ya umma; lakini haijumuishi wanaoshikilia nafasi hizo kwa
sehemu ya muda wa ziada(Part Time basis).MSIKILIZE MAMA BISIMBA , NILIPOZUNGUMZA NAE KUHUSU HILI
Subscribe to:
Posts (Atom)