Monday, August 13, 2012

NIMEICHAGUA HII KATIKA MTANDAO ... KUWA PICHA YA MWAKA YA WAPENDANAO

HUYU JAMAA ANAITWA NICKY... kwa mujibu wa ushuhuda ambao upo katika video ambayo nimewahi kuitazama, alizaliwa akiwa hana mikono wala miguu. Yeye anamshukuru Mungu kila siku kwa kuwa alimuumba hivyo..... 
Jamaa anajua kusoma , na kuandika kwa kutumia kompyuta, pia jamaa huyu ni muhubir, kwenye ushuhuda wake niliona akitoa neno la Mungu.
Maisha yake yaliyo katika ushuhuda huo wa video, anafanya mambo meengi yeye mwenyewe, mfano anapiga mswaki, ananyoa ndevu, na anaifunua biblia yeye mwenyewe.....
Picha hii inamuonesha bwana huyu, akiwa na mpenzi wake , mtu ambaye amejitolea maisha yake kwa ajili ya upendo wa dhati, na hakujali vile alivyo bali bila shaka alizingatia upendo wa dhati alionao Nick..
Nitakuwekea video yake uitazame katika ushuhuda...... KWELI HAKUNA LISILOWEZEKANA

AMA WAWEZA GUSA HAPA KUUONA USHUHUDA WA NICKY

No comments: